ISRAELI-PALESTINA-MAREKANI

Kerry kurejea tena Mashariki ya Kati juma lijalo

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani  John Kerry
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry REUTERS/Yuri Gripas

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry anatarajiwa kurejea tena katika eneo la Mashariki ya kati juma lijalo, ambapo Kerry atakutana na waziri mkuu wa Israel Banjemin Netanyahu ambaye amekosoa vikali makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran yaliyofikiwa hivi karibuni mjini Geniva. 

Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hiyo, Kerry pia atazungumza na rais Mahamud Abbas katika mwendelezo wa jitihada za kushawishi kusonga mbele kwa mazungumzo ya amani baina ya Israel na Palestina.

Mwanzoni mwa mwezi huu Kerry alizuru Mashariki ya kati kabla ya kuelekea Geneva kwenye mazungumzo ya nyuklia ya Iran ambayo yaliandika historia ya kipekee katika karne hii baada ya kufanikiwa kufikia makubaliano ya awali juu ya urutubishaji wa uranium huko Tehran.

Marekani na Mataifa yenye nguvu duniani wanasema makubaliano hayo yatasaidia kuhakikisha usalama wa eneo la Mashariki ya kati na dunia kwa ujumla.