KENYA-ICC

Mahakama ya ICC huenda ikaruhusu kesi ya Kenyatta na Ruto kuendeshwa kwa njia ya video baada ya nchi wanachama wa ICC kukubaliana kuhusu hilo

Rais Uhuru Kenyatta  akiwa na naibu wake William Ruto
Rais Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto Reuters/Presidential Strategic Communications Unit

Hatimaye nchi wanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC wamekubali kesi inayowakabili viongozi wa Kenya kuendeshwa kwa njia ya video.

Matangazo ya kibiashara

Awali rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliitaka ICC na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuahirisha mashtaka yao dhidi ya uchochezi wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Hivi karibuni mahakama hiyo iliarifu kuwa ni sharti Kenyatta afike mjini Hague kusikiliza kesi yake na ushahidi unaotolewa dhidi yake, na endapo kutakuwa na suala linalomzuia kuhudhuria basi litatazamwa kwa kuzingatia uzito wake.

Wanachama 122 wa mahakama hiyo pia wamelegeza masharti mengine dhidi ya mashtaka yanayowakabili viongozi wa kisiasa, suala ambalo linatafrisiwa kama ushawishi toka kwa nchi za Kiafrika zinazotetea viongozi wanaokabiliwa na mashataka katika mahakama hiyo.

Baadhi ya nchi za Afrika zinazidi kuikosoa mahakama ya ICC kwa madai kuwa inakandamiza viongozi wa bara hilo.