Umoja wa Mataifa-UNICEF

Maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa watoto yapungua maradufu ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita

Maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa watoto yapungua maradufu ukilinganishwa na miaka 10 iliyopita.
Maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa watoto yapungua maradufu ukilinganishwa na miaka 10 iliyopita. ertagov.com

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa kupinga maambukizi ya virusi vya UKIMWI,ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa maambukizi mapya kwa watoto yamepungua maradufu ukilinganishwa na miaka 10 iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inasema kuwa toka mwaka 2005 maambukizi mapya kwa watoto wadogo yamepungua ambapo watoto zaidi ya laki 8 na elfu 50 waliondolewa kwenye hatari ya kupata maambukizi hayo huku ripoti hiyo ikionya kuongezeka kwa maambukizi mapya kwa vijana iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Shirika la Umoja wa mataifa linalishughulikia watoto UNICEF linasema kuwa idadi ya vifo kwa watoto walio na umri wa kati ya miaka 10 hadi 19 imeongezeka kwa asilimia 50 kati ya mwaka 2005 na 2012 ikiongezeka kutoka vifo elfu 71 hadi laki 1 na elfu 10.

UNICEF imeongeza kuwa hata hivyo maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito yamepungua kutokana na mataifa mengi kutenga fungu la kutosha kukabiliana na ugonjwa huo.

Kila tarehe mosi mwezi Desemba dunia huadhimisha siku ya ukimwi kimataifa.