ISRAEL-PALESTINA-MAREKANI

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry awasili Israel kwa mazungumzo na waziri mkuu Benjamin Netanyahu

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani  John Kerry
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry REUTERS/Yuri Gripas

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry amewasili nchini Israel jana jioni, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kuifanya nchini humo toka kufikiwa kwa makubaliano kati ya mataifa ya Magharibi na nchi ya Iran kuhusu mpango wake wa Nyuklia hatua iliyougadhabisha utawala wa Israel. 

Matangazo ya kibiashara

Ziara ya waziri Kerry nchini Israel inalenga kuendelea na juhudi za taifa hilo kuhusu kufufua upya mazungumzo ya amani kati ya taifa hilo na Palestina kuhusu eneo la ukingo wa Magharibi na Jerusalem ambalo linagombewa na nchi hizo.

Hii leo waziri Kerry atakutana kwa mazungumzo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kabla ya kusafiri kwenda mjini Ramallah ambako atakutana na rais Mahmoud Abbas ambapo suala la nyuklia la Iran na eneo la ukanda wa gaza linatarajiwa kuwa kwenye ejenda kuu ya mazungumzo ya Kerry na viongozi hao.

Waziri mkuu Netanyahu, amekuwa mkosoaji mkubwa wa mataifa matano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama ikiwemo Ujerumani, kwa uamuzi wao wa kukubalia kuilegezea masharti Iran baada ya kukubali vinu vyake kukaguliwa.