YEMEN

Al Qaeda ladai kutekeleza shambulizi nchini Yemen na kuua 52

Kundi la Al Qaeda lakiri kutekeleza Shambulizi nchini Yemen na kuua watu 52
Kundi la Al Qaeda lakiri kutekeleza Shambulizi nchini Yemen na kuua watu 52

Kundi la kigaidi la Al-Qaeda limejitokeza siku ya Ijumaa na kujigamba kutekeleza shambulizi nchini Yemeni lililoua watu 52,limebainisha hayo katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wake.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi katika wizara ya ulinzi nchini Yemen lilitekelezwa siku ya alhamisi baada ya wapiganaji wa kijahidina kuthibitisha kwamba wamedhibiti vumba vya kuongoza ndege zisizokuwa na rubani na wataalamu wakimarekani.

Miongoni mwa waliopoteza maisha katika shambulizi hilo ni pamoja na madaktari wawili raia wa Ujerumani,wawili kutoka Vietnam, Yemen na wauguzi wawili kutoka Ufilipino na mmoja kutoka India.

Taarifa ya awali ilibainisha kuuawa kwa madaktari sita raia wa Venezuela,wawili wa Ufilipino na watatu wa Yemen.

Shambulizi hilo pia limesababisha majeruhi kufikia 167 huku tisa miongoni mwa hao ni mahututi.