JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Wanajeshi wa Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, waanza zoezi la kupokonya waasi silaha,huku changamoto za kuwatambua zikitatiza zoezi hilo

Wanajeshi wa Ufaransa wakifanya doria kwenye mji mkuu Bangui nchini Afrika ya Kati
Wanajeshi wa Ufaransa wakifanya doria kwenye mji mkuu Bangui nchini Afrika ya Kati www.voanews.com

Wanajeshi wa Ufaransa wameanza zoezi la kuwapokonya silaha wapiganaji waasi huko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kama ilivyokuwa imepangwa jana Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Awali kuliarifiwa makabiliano makali kati ya wanajeshi hao na wapiganaji wa serikali mjini Bangui, wakati shughuli hiyo ilipoanza.

Hata hivyo zoezi hilo limetajwa kuwa gumu kutokana na kwamba waasi wa seleka wamevua sare zao na kujichanganya na raiaa na hivyo kuwa vigumu kuwatambua kwa haraka.

Kikosi cha wanajeshi 1,600, wa Ufaransa kimepelekwa nchiniJamhuri ya Afrika ya Kati baada ya siku kadhaa za mapigano yaliyosababisha vifo vya watu 400.

Wanajeshi hao wa Ufaransa, sasa wanashika doria katika barabara na mitaa yote ya mji mkuu Bangui huku Umoja wa Afrika nao ukiahidi kuongeza mara mbili ya wanajeshi wake nchini humo ili kurejesha amani nchini humo.