BANGLADESH

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Bangladesh aziwiliwa kutotoka kwenye makaazi yake

Upinzani nchini Bangladesh umeituhumu serikali ya nchi hio kumpa adhabu ya kifungo cha nyumbani kiongozi wao, baada ya kutoa wito wa kufanya maandamano dhidi ya chaguzi za wabunge na wanaseneti zitakazofanyika chini ya ulinzi mkali wa jeshi. Waziri wa zamani, Khaleda Zia, amepanga kuandaa maandamano tarehe 29 mwezi desemba katika mji wa Dhaka, ili kulani kufanyika kwa chaguzi, ambazo zimepangwa kufanyika tarehe 5 mwezi wa januari, huku vyama 21 vikisema kwamba vitasusia chaguzi hizo.

Matangazo ya kibiashara

Khaleda Zia, ambae ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Bangladesh, the Bangladesh Natuonalist Party (BNP), amewekwa kwenye kifungo cha nyumbani toka jana, amesema kiongozi m'moja wa chama chake.

“Polisi hairusu mtu yeyote kuongea nae, hata viongozi na wafuasi wa chama cha BNP hatua hio inawahusu. Hatua hio ya serikali inakuja kuzuiya maandamano ya kuunga mkono demokrasia ambayo yamepangwa kufanyika tarehe 29 mwezi wa desemba”, amesema naibu kiongozi wa BNP, Shamsher Mobin Chowdhury.

Polisi kwa upande wake, imesema imefanya hivo ili kuimarisha usalama wa Khaleda Zia, huku ikithibitisha kukamatwa kwa viongozi wawili wa BNP mbele ya makaazi ya Zia. Polisi imekanusha madai ya kwamba imeongeza idadi ya askari polisi kwenye makazi ya Zia ili kupiga marufuku kwa mtu yeyote kuongea na Khaleda Zia.

Kiongozi huyo wa upinzani, ambae aliwahi kua waziri mkuu mara mbili, alitolea wito wafuasi wake jana kuandamana jumapili kwa kusema “hapana' kwa uchaguzi usiyoeleweka na kusema “ndio” kwa demokrasia.

Upinzani umekua ukisisitiza kwa miezi kadhaa uundwaji wa serikali ya mseto itakayo andaa chaguzi, lakini waziri mkuu wa Sheikh Hasina amepinga jambo hilo.

Katika hali hio ya mvutano, wanajeshi watatumwa katika vitongoji takribani 59 kwa jumla ya vitongoji 64 nchini kote.

Msemaji wa tume ya uchaguzi, S.M. Asaduzzaman, amesema wanajeshi hao watatumia nguvu iwapo kutatokea uhasama, na watapiga doria katika maeneo muhimu na kwenye mabaraba.

Kwa upande wake msemaji wa jeshi, Muhammad Reza-ul Karim, amesema kundi la kwanza la wanajeshi lilitumwa mwanzoni mwa juma hili, na wamepanga kuanza shughuli zao leo alhamisi.

“Wanajeshi wametumwa katika vitongoji hivyo kwa ombi la tume ya uchaguzi ili kuhakikisha chaguzi zimekua huru, amesema Muhammad Reza-ul Karim.

Chama cha BNP kimelani kutumwa kwa wanajeshi hao, kikibaini kwamba hali hio itasababisha raia wanakua na wasiwasi.

Mazungumzo yaliyoitishwa hivi karibuni chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa kwa kutafuta mkataba kati ya chama tawala, Awami League, na BNP yalikwenda kombo.

Pande hizo mbili zimekua zikituhumiana kuhusika na kupandikiza chuki kati ya raia.