SUDANI KUSINI

Hali yatatanisha nchini Sudan Kusini baada ya kila upande kudai kuudhibiti mji muhimu wa Malakal

Majeshi ya serikali ya Sudan Kusini na waasi, kila upande unadai kudhibiti mji muhimu wa Malakal. Hayo yanajiri wakati zimeanzishwa mjini Nairobi jitihada mpya za kidiplomasia kujaribu kuzuia mgogoro katika nchi hio changa." Mji wa Malakal uko chini ya udhibiti kamili wa vikosi vinavyomtii aliyekuwa makamu wa Rais, Riek Machar, " amesema Moses Ruai , msemaji wa waasi, na kuongeza kuwa vikosi vya serikali viliondoka katika mji huo jana alhamisi usiku.

Matangazo ya kibiashara

Mji huu unaopatikana kaskazini mwa nchi ni mji mkuu wa jimbo la Upper Nile, ambao ni tajiri kwa mafuta. Jeshi la serikali linapambana na waasi tangu jumatatu.

Waziri wa ulinzi wa Sudan Kusini , Kuol Manyang Juuk , amesema kwamba hizo ni habari potovu, na kudai kwamba waasi walishindwa, na kuamua kukimbia. “Mji wa Malakal kwa sasa uko chini ya udhibiti wa vikosi vya serikali”, amesema Manyang Juuk.

Sudan Kusini, tangu Desemba 15 inakabiliwa na mapigano makali, ambayo yanatishia kuenea nchi nzima na kugeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Chanzo cha mgogoro huu, ni upinzani kati ya Rais Kiir na aliyekuwa Makamu wake, ambaye aliachishwa kazi mwezi Julai.

Rais Salva Kiir anamtuhumu aliekua makamo wake jaribio la mapinduzi, huku Riek Machar akikanusha tuhuma hizo, akibaini kwamba Salva Kiir anapanga kuwamalizia maisha wapinzani wake .

Waasi walichukua udhibiti wa miji mingine mikuu ya mikoa, Bentiu katika Jimbo la mafuta la Unity na Bor katika jimbo la Jonglei kabla ya kuanguta mikononi mwa jeshi la serikali jumaine iliyopita.

Migogoro ya hivi karibuni katika taifa changa, huru la Sudan inachochewa na malumbano ya muda mrefu kati ya vigogo wawili, rais Salva Kiir na aliekua makamu wake Riek Machar, lakini pia muelekeo wa kikabila :Dinka kabila ya Salva Kiir dhidi ya Nuer, ambalo ni kabila la Riek Machar.

Salva Kiir na Riek Machar walikubaliana kuanza mazungumzo , lakini bila kuweka tarehe . Na mapigano bado kufikia angalau nusu ya majimbo 10 ya nchi, ikiwa ni pamoja na Jonglei, Unity , Ecuador ya kati ( Juba ), lakini pia Nile na miji mingine