Lebanon-mashambulizi

Majeshi ya Lebanoni yajibu mashambulizi ya helikopta za jeshi la Syria katika ardhi yake

Wakimbizi wa Syria waliokimbilia nchini Lebanono wakipewa msaada wa chakula
Wakimbizi wa Syria waliokimbilia nchini Lebanono wakipewa msaada wa chakula REUTERS/Omar Ibrahim

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mzozo wa Syria, jeshi la Lebanoni limejibu mashambulizi ya makombora yaliorushwa na jeshi la Syria na kuangukia katika eneo la mashariki mwa Lebanoni bila hata hivyo kusababisha hasara yoyote.

Matangazo ya kibiashara

Huu ni ujumbe mzito wa jeshi la Lebanon linalo tuhumiwa kuwa dhaifu dhidi ya mashambulizi yanayoendeshwa na vikosi vya majeshi ya Syria katika mpaka na taifa hilo.

Helikopta za kijeshi zilirusha risase zilizoangukia katika ardhi ya Lebanon bila hata hivyo kusababisha hasara yoyote, tukio lilifuatiwa na mashambulizi ya makombora ya jeshi la Lebanon ambayo pia hayakusababisha asara yoyote.

Mwezi Juni iliopita jeshi la Lebanon liliitahadharisha Syria kwamba haitosalia kimya katika mashambulizi yake. Tahadhari ambayo hadi leo ilikuw abado haijatekelezwa na ambapo wataalamu wanasema kwamba asilimia kubwa ya majeshi ya Lebanon yanaunga mkono Utawala wa Assad

Licha ya jibu hilo la vikosi vya Lebanon, wachambuzi wa maswala ya kijeshi wanaokuwa majeshi ya Lebanon hayana uwezo wowote wa kuzuia mashambulizi ya aina yoyote na kwamba tukio hilo ni kutaka kujiosha mbele ya jumuiya ya kimataifa na wanasiasa nchini humo ambao wanalituhumu jeshi la nchi hiyo kuunga mkono utawala wa Syria.

Wananchi na wanasiasa nchini humo wamegawanyika sehemu mbili kufuatia mzozo wa Syria ambao unaendelea kugharimu maisha ya wananchi na ambao Jumuiya ya Kimataifa imeshindwa kuutatua kwa njia ya kidiplomasia kufiatia pia kugawanyika kwa wajumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mzozo huo.

Ma elfu ya wananchi nchini Syria wameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Lebanoni kufuatia mapambano yanayoendelea kati ya majeshi ya serikali na yale ya waasi wa jeshi huru nchini Syria.