PALESTINA-IRAEL

Israeli na Palestina kila upande unashutumu mwengine kwa kukwamisha mchakato wa amani

Israeli na Palestina zinatupiana lawama ya kuvuruga juhudi za mchakato wa amani wakati huu waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry akifanya ziara katika eneo la mashariki ya kati. Katika ziara hiyo ya kumi ya kiongozi huyo tangu mwezi March katika eneo hilo la mashariki ya kati, John Kerry anatarajia kuongeza kuwahimiza viongozi wa Palestina na Israeli kuendeleza mazungumzo wakati huu kukiwa na hali ya sintofahamu kati ya pande zote mbili

Matangazo ya kibiashara

John Kerry atakutana kwa mazungumzo na waziri mkuu Benjamin Netanyahu alhamisi hii na kugusia mambo kadhaa ambayo yanakwamisha maendeleo ya mazungumzo hayo.

Baadae kesho Ijumaa Kerry atakutana na rais wa Mamlaka ya wa Palestina mjini Ramallah, huko Scijordania.

Kubwa zaidi linalo kwamisha mazungumzo baina ya pande hizo mbili ni ujenzi wa makaazi ya wayahudi wa kilowezi katika eneo la Jerusalem kaskazini na Scijordania, pamoja na swala la wafungwa.

Hivi karibuni Mahmoud Abbas alitishia kuchukuwa hatuwa za kisheria na kidiplomasia dhidi ya Israeli, ambayo inaendelea kujenga majumba 1.400 ambapo ujenzi wa majumba hayo utatangazwa baada ya ziara ya John keery katika ukanda huo.

Ndoto za kufikiwa amani katika mashariki ya kati kwa miongo kadhaa zimekuwa zikitiliwa juhudi na Marekani lakini ziligonga mwamba tangu mwezi Septemba mwaka 2010.

Hii si mara ya kwanza mazungumzo hayo yanaanzishwa. Awali  Palestina na Israel walifanya mazungumzo mwezi wa saba mwaka 2013, jijini Washington nchini Marekani, huku viongozi wa pande zote wakielezwa kuwa tayari kufanya maamuzi magumu katika kuelekea kupatikana amani.