SOMALIA-Mashambulizi

Milipuko miwili yagharimu maisha ya watu mjini Mogadishu nchini Somalia

Takriban watu nane wamepoteza maisha, wengi wao wakiwa ni wanajeshi katika milipuko miwili ya kujitowa muhanga iliotokea jana jioni mjini Mogadishu kwa nyakati tofauti. Duru za polisi zimearifu kuwa mlipuko huo wa pili umetokea wakati walinzi wa usalama walipokuwa katika harakati za kuwaokowa watu waliokumbwa na shambulio la bomu la kujitowa muhanga karibu na Hotel Jazeera.

M'moja kati ya majeruhi aondolea eneo la tukio mjini Mogadishu
M'moja kati ya majeruhi aondolea eneo la tukio mjini Mogadishu
Matangazo ya kibiashara

Mashahida wamesema kulitokea na ubadilishanaji wa risase baina ya wanajeshi wa serikali na washambuliaji

Ali Ibrahim mmoja kati ya mashuhuda amesema watu watano ambao ni miongoni mwa washambuliaji wamepoteza maisha.

Takriban watu watano walipoteza maisha siku ya Ijumaa iliopita katika shambulio kama hilo jijini Mogadishu.

Duru za polisi ziliarifu kuwa bomu lillilotegwa karibu na barabara katika eneo la mgahawa ambako wanajeshi wa Somalia walipokuwa wakipumzika na kulituhumu kundi la Al Shabab kuhusika na shambulio hilo.

Hakuna kundi lolote ambalo limejigamba kuhusika na shambulio hilo.

Kundi la Al Shabab limekuwa likiendesha mashambulio ya kujitowa muhanga katika miaka hii miwili ya nyuma, tangu pale lilipo furushwa katika mji wa Mogadishu na majeshi dhaifu ya serikali yakisaidiwa na vikosi vya Umoja wa Afrika nchini humo Amisom.