RWANDA-AFRIKA KUSINI

Serikali ya Rwanda yanyooshewa kidole kuhusika na Kifo cha Aliekua mkuu wa idara ya ujasusi nchini Rwanda P. Karegeya

Kanali Patrick Karegeya, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi katika miaka ya 1994 hadi 2004
Kanali Patrick Karegeya, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi katika miaka ya 1994 hadi 2004

Wafuasi wa vyama vya upinzani nchini Rwanda walioko ukimbizini wamefahamisha usiku wa kuamkia leo alhamisi, kifo cha Patrick Karegeya, mkuu wa idara ya ujasusi nchini Rwanda hadi mwaka 2004 kabla ya kupoteza imani kwa rais wa Rwanda Paul Kagame, na kukimbilia nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa mkuu wa zamani wa majeshi nchini Rwanda, jenereli Kayumba Nyamwasa, ambae anaeshi pia ukimbizini nchini Afrika kusini, Patrick Karegeya amepatikana amechomwa visu katika chumba cha hoteli iitwayo Michelangalo Towers, katika tarafa ya Sandton, mjini Johannesburg.

Matangazo ya kibiashara

Mchana wa tarehe 31 disemba, Patrick Karegeya alimfahamisha m'moja kati ya watu waliyokutana nae kwamba atapashwa kumuona kwa mazungumzo baadae, rafiki yake wa muda mrefu.

Baadae aliwafahamisha jamaa zake kwamba ana ahadi na rafiki yake wa muda mrefu, ambae anajulikana kwa jina Apollo, jioni kwenye hoteli Michelangelo Towers.

Jamaa zake waliwasiliana nae mara ya mwisho saa moja na nusu usiku, na toka muda huo, mawasiliano kati ya mkuu huyo wa zamani wa idara ya ujasusi nchini Rwanda na jamaa zake yalikosekana.

Jamaa na marafiki wa Patrick Karegeya wanautuhumu utawala wa Rwanda kuhusika na kifo hicho.

Mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda, jenerali Kayumba Nyamwasa, alie ukimbizini nchini Afrika Kusini, ambae pia alikosewa kuuwawa katika mazingira kama hayo mwaka 2010, amesema kwamba ni mauwaji ya kisiasa.

“Sina shaka na tukio hili, serikali ya Rwanda inahusika na kifo cha Patrick Karegeya.

Marehemu hakua na ugomvi na mtu yeyote hapa Afrika Kusini, isipokua rais Paul Kagame , ambae alimfuatila ili amuangamize kwa kipindi chote hiki cha miaka kumi iliyopita.

Haya ni mauwaji ya kisiasa, kama jinsi serikali ya Rwanda imekua ikifanya kwa wapinzani wake”, amesema jenerali Kayumba Nyamwasa.

Patrick Karegeya ameishi Afrika Kusini kwa kipindi cha miaka sita.

Mkuu huyu wa zamani wa idara ya ujasusi katika miaka ya 1994 hadi 2004, aliwahi kua mshirika wa karibu wa rais Paul Kagame, kabla ya kupoteza imani.

Aliwekwa jela mara mbili, na baadae mwaka 2007, aliamua kukimbilia ukimbizini.

Il avait accusé le président Kagame d’avoir organisé l’attentat contre l’avion du président Habyarimana, considéré comme l’élément déclencheur du génocide de 1994.

À l’époque, Patrick Karegeya s’était même dit prêt à coopérer avec la justice française, en charge de l’enquête.

Patrick Karegeya aliwahi kumshutumu rais Paul Kagame kwamba alipanga njama ya kuilipua ndege aliyokuemo mtangulizi wake, rais Juvenal Habyarimana, akilaumu kwamba, Paul Kagame ndie chanzo cha mauwaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.

Serikali ya Rwanda haijatoa tangazo lolote linalohusiana na kifo hicho.