JAMUHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO-Usalama

Hali ya usalama yaendelea kudorora katika baadhi ya maeneo ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Serikali ya Kinshasa imekanusha taarifa za kutokea kwa mashambulizi katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Ndolo hapo jana jioni jijini Kinshasa, ikiwa ni siku tatu baada ya kushuhudiwa kwa mashambulizi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa njili, na vituo vingine vitatu muhimu. 

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Mende amesema kwamba milio ya risase ilisikika karibu na uwanja huo wa ndege baada ya mwanajeshi mlinzi wa kiwanda kimoja katika eneo hilo kurusha risase hewani wakati akiwafukuzuia majambazi waliokuwa na nia ya kuendesha wizi.

Hayo yanajiri wakati wananchi wa taifa hilo hususan wale wa mashariki mwa DRCongo wakikumbwa na simanzi kufuatia kifo cha kiongozi wa operesheni za kijeshi katika mkoa wa kivu kaskazini Kanali Mamadou Ndala Mustafa aliye uwawa jana katika shambulio la kuvizia.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Lambert Mende gari alilokuwemo kanali Mamadou Ndala lilipigwa Roketi na kundi la waasi wa Uganda wa ADF-NALU.

Mashirika ya kiraia mashariki mwa DRCongo hii leo yamewatolea wito wananchi wa maeneo hayo kutokwenda kazini kama ishara ya kumkumbuka shujaa huyo ambaye wanasema aliwakomboa dhidi ya uasi wa kundi la M23.

Kanali Mamadou Ndala atakumbukwa sana na wananchi wa Goma, baada ya mwezi Julay kukabiliana na waasi wa kundi la M23 waliokuwa na lengo la kuuteka mji wa Goma, na ambapo Ndala na kikosi chake waliendesha mapigano hadi kufikia kuutokemeza uasi wa M23 mwishoni mwa mwezi novemba mwaka 2013.

Nyuso za wananchi wa maeneo na mashariki mwa DRCongo, zimejawa na simanzi huku wengi wakiomba uchunguzi uanzishwe mara moja kubaini mazingira ya kifo cha kamanda huyo.