MADAGASCAR-Matokeo ya uchaguzi

Tume ya Uchaguzi nchini Madagascar yamtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais

Herry Rajaonarimampianina, ambae anaungwa mkono na utawala unaomaliza muda wake, ameshinda uchaguzi wa rais nchini Madagascar, kwa mujibu wa taarifa ya mwisho iliyotolewa Ijumaa , lakini uthibitisho wa ushindi wake utategemea na uamuzi wa mahakama iliokabidhiwa kufikiria maombi kwa uvunjaji kesi iliyowasilishwa mahakamani hivi karibuni na mpinzani wake, Robinson Jean Louis.

Matangazo ya kibiashara

Herry Rajaonarimampianina, ametoa wito wa kujizuia kwa kusubiri uamuzi wa mahakama, ambao unatazamiwa kutolewa ndani ya wiki mbili : "ninatolea wito raia wa Madagascar kua watulivu kwa kusubiri matokeo ya mwisho ," amesema leo asubuhi, Herry Rajaonarimampianina, baada ya kutangazwa mshindi.

Herry Rajaonarimampianina, mwenye umri wa miaka 55 , ambae pia waziri wa zamani fedha katika serikali ya " mpito " ameshinda kwa kura asilimia 53.50 dhidi ya mpinzani wake Herry Rajaonarimampianina, ambae amepata asilimia 46.50 ya kura.

Jean Louis Robinson, amekua akiungwa mkono na rais wa zamani wa Madagasar alietimuliwa Marc Ravalomanana.

Jean Louis, anaedai kua uchaguzi wa tarehe 20 desemba, uligubikwa na wizi wa kura, amesusia sherehe za ktangaza matokeo ya uchaguzi, ziliyofanyika kwenye makao makuu ya Tume ya Uchaguzi ( Cenit ).

"Sikusikiliza tangazo la matokeo ya uchaguzi liliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ( Cenit ), kwa hio sijui kinachoendelea, mimi bado nasubiri uamzi wa Mahakama Maalumu ya Uchaguzi " amesema Jean Louis Robinson, akiambia AFP kwa njia ya simu.

Akiungwa mkono na rais wa zamani Marc Ravalomanana aliepinduliwa mwaka 2009 , Jean Louis aliwasisha mahakamani zaidi ya maombi mia yanayokemea " udanganyifu, na makosa " viliyogubika uchaguzi huo, na kuomba kutoidhinisha uchaguzi.

Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina walitakiwa na Jumuiya ya Kimataifa kutogombea kwenye uchaguzi wa urais kwa kuhofia machafuko, kila m'moja aliamua kuunga mkono m'moja kati ya wagomebea waliyofaulu kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi.