SUDANI-SUDAN KUSINI-Diplomasia

Mataifaya Sudan na Sudan Kusini yakubaliana kuunda jeshi la pamoja la kulinda visima vya mafuta kusini mwa Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini Salva kiiir na Mwenzake wa Sudan Omar Al Bashir wamekubaliana kuunda jeshi la pamoja kulinda maeneo yenye utajari wa mafuta katika katika mipaka ya mataifa hayo mawili kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya waasi na aliyekuwa Makamu wa Rais Riek Machar na majeshi ya serikali

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Sudan Ali Ahmed amesema kuwa marais hao walikubaliana kuunda jeshi hilo wakati wa mashauriano yao siku ya Jumatatau jijini Juba kuhusu mzozo unaoendelea nchini Sudan Kusini.

Taarifa hii inakuja baada ya Rais wa Sudan Omar Bashir kwenda mjini Juba kwa mashauriano na Rais Salva Kiir kuhusu mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.
Mgogoro huo ni kati ya wafuasi wa Rais Kiir na hasimu wake Riek Machar aliyekuwa makamu wa rais wa Salva Kiir ingawa alifutwa kazi pamoja na mawaziri wengine wa serikali.

Bashir alizuru Juba wakati wajumbe wa serikali na waasi wakianza mazungumzo ya ana kwa ana jijini Addis Ababa kujaribu kumaliza vita katika taufa hilo changa.

Rais Salva Kiir kwa mara nyingine amewakemea waasi anaosema walikuwa na mpango wa kumwondoa madarakani, na kuongeza kuwa wanastahili kujitokeza na kuomba radhi.

Machafuko nchini Sudan Kusini yamesababisha zaidi ya watu elfu moja kupoteza maisha na maelfu kukimbia makwao, na raia wa kigeni kurudi makwao.