JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI-Dilpomasia

Ufaransa haikubaliani na madai ya kuongezwa kwa wanajeshi wake nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati

RFI

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema hakuna haja kwa sasa kuongeza ididi ya wanajeshi wa Ufaransa katika Jamhuri ya Afria ya Kati kusaidia kutuliza mapgano ya kidini yanayoendelea. Kwa sasa Ufaransa ina wanajeshi 1,600 nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati waliyotumwa kupokonya silaha makundi ya Seleka na Anti-balaka, ambayo yamekua yakinyooshewa kidole kwamba yanahusika na mauwaji yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Ufaransa limekua likilaumiwa na baadhi ya raia wa Jamuhuri ya Afrika ya kati hasa waislamu kwamba linaegemea upande wa wakristo, na kubaini kwamba jeshi hilo haliwajibiki vilivyo kwa kazi yake, hasa kufumbia macho vitendo vya mauwaji vinavyofanywa na kundi la vijana wa kikristo, Anti-balaka, dhidi ya waislamu.

Hata hivyo, Le Drian amesema kuwa ikiwa kutakuwa na haja ya kuongeza wanajeshi zaidi, hilo litafanyika baada ya wanajeshi wa Afrika chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa kupewa jukumu kamili la kuendeleza Operesheni ya kulinda amani mwezi ujao.

Mwishoni mwa mwezi wa desemba, rais wa kipindi cha mpito nchini Jamhuri ya Afrika ya kati Michel Djotodia pamoja na viongozi wa kidini waliwatolea wito wananchi wa taifa hilo wa kuachana na mauaji na badala yake kupendana na kuepusha tofauti zao za kidini na kuendelea kueshi kwa ushirikiano kama ilivyokuwa miaka ya hivi karibuni.

Wananchi wa Afrika ya Kati wanakabiliwa na ukosefu wa usalama na maelfu wamekimbia makwao, kipindi hiki majeshi ya Ufaransa na yale ya Umoja wa Afrika yakiendeleza Opereshenii ya kuyapokonya silaha makundi ya wapiganaji na kulinda amani.

Mapigano ya kidini nchini humo yamesabaisha maelfu ya watu kupoteza maisha.