JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI-Dilpomasia

Viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya Mataifa ya Afrika ya Kati wakutana jijini N'Djamena kujadili hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

RFI

Viongozi wa mataifa jirani ya nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wanakutana kwa mazungumzo mjini N'Djamena ili kumshininikiza rais Michel Djotodia arejeshe usalama katika taifa lake, ambalo linakumbwa na machafuko. Akifungua mkutano huo wa Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika ya Kati (CEEAC) ,rais wa Chad, Idriss Déby Itno, ambae ni mwenyekiti wa Jumuiya hio, amewataka wanaoshiriki mkutano kusalia kimya kwa muda wa dakika moja kutokana na hali inayokumba raia wa kiafrika nchini Jamhuri ya afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

“Sote tutuzame hali inayojiri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati: Taifa hilo linakabiliwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe, ambao walilitumbukiza katika vita hatari vya kidini”, amesema Déby.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia na waziri mkuu Nicolas Tiangaye wanahudhuria mkutano huo.

“Tunapashwa kuonesha zaidi mshikamano na msimamo wetu ili Jamhuri ya Afrika ya Kati iondokane katika hali inayoikabili kwa sasa. Inatubidi tuwe na uamzi fika”, amesema rais wa Chad kabla ya ya shughuli za faragha kuanza.

Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika ya Kati, mkiwemo Chad ambayo ni taifa jirani, yanapania kuresha amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

“Kutokana na hali inayojiri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Serikali ni dhaifu, na haina uwezo wa kurejesha utulivu, kuna uwezekano wa wa kunda seikali itakyowashirikisha wanasiasa wote, lakini tusubiri tuone uamzi utakaochukuliwa na ndugu zetu wafrika”, amesema waziri wa mashauri ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius kwenye televisheni France 2, huku akijizuia kusema kua, kujiuzulu kwa Michel Djotodia kutasaidia hali ya usalama kurejea kuwa nzuri.

Hata hivyo, Msemaji wa rais Djotodia, Guy Simplice Kodégué amekanusha madai ya kujiuzulu kwa Mchel Djotodia.