UFARANSA-MALI

Ufaransa iko mbioni kupunguza idaidi ya wanajeshi wake wanaolinda amani nchini Mali

REUTERS/Philippe Wojazer

Rais Francois Hollande amesema kuwa kwa sasa hali imeanza kurejea kama kawaida Kaskazini mwa Mali na Operesheni yao ya kupambana na makundi ya kigaidi imefanikiwa pakubwa. Ufaransa ilizundua Opereshni inayofahamika kama Serval mwezi Janauari mwaka moja uliopita.  

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao wanao kadiriwa 2,500 watapunguzwa hadi kufikia 1,600 kufikia katikati ya mwezi wa februari

Mwanzoni mwa mwezi wa novemba, kundi la Al Qaeda tawi la ukanda wa Maghreb, lilijigamba kuhusika katika mauaji ya waandishi wa habari wawili raia wa Ufaransa novemba 2 mjini Kidal kaskazini mashariki mwa Mali, na kudai kuwa ni ulipizaji kisasi kwa vitendo vya wanajeshi wa Ufaransa wanaowafanyia wenzao huko kaskazini mwa Mali.

Katika taarifa iliotolewa na mtandao mmoja nchini Mauritania wa Sahara Medias, kundi la Al Qaeda eneo la Maghreb (Aqmi) lilithibitisha kuwa mauaji hayo yalitekelezwa ili kujibu mapigo ya maumivu wanayoyapata raia wa Mali kutoka kwa wanajeshi wa Ufaransa na wale wa Umoja wa Afrika katika eneo la Azawad.

Ghislaine Dupont mwenye umri wa miaka 57 na Claude Verlont mwenye umri wa miaka 55 waandishi wa habari wa RFI waliuawa katika eneo la kilometa chache na mji wa Kidal muda mfupi baada ya kutekwa na kundi ndogo la watu waliokuwa wamejihami kwa silaha.

Hata hivyo, aliyekuwa zamani katibu mkuu wa Umoja wa mataifa UN, Kofi Annan, aliipongeza serikali ya Ufaransa kujituma katika kusuluhisha migogoro ya kivita inayoendelea kuenea barani Afrika.

Akiwa ziarani jijini Paris nchini Ufaransa, Anan alisema kitendo cha Ufaransa kuwatuma wanajeshi wake nchini Mali lakini pia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ni mfano unaofaa kuigwa na mataifa mengine duniani.