SUDANI KUSINI

Mapigano yanaendelea nchini Sudan Kusini wakati mazungumzo ya kusaka amani yakisuasua mjini Addis Ababa

Umoja wa Mataifa unasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha katika mapipagno yanayoendelea nchini Sudan Kusini imefikia kwa sasa zaidi ya elfu moja. Wakati Umoja wa Mataifa ukisema hayo, waasi wanasema wameimarisha ngome zao katika mji wa Bnetiu ambao wamekuwa wakiushikilia kwa muda sasa huku majeshi ya serikali yakisema yanakaribia kuudhibiti. 

RFI
Matangazo ya kibiashara

Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia mazungumzo ya kusitisha mapigano bado yanaendelea kwa mwendo wa kinyonga huku kila upande ukishikilia msimamo wake.

Waasi wanataka kuachiliwa kwa washirika 11 wa kiongozi wao Riek Machar ili kufaniksiha mazungumzo hayo ombi ambalo rais Salva Kiir amekataa.

Riek Machar anasema mapigano yataendelea.

Naye kiongozi wa Majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani, Herve Ladsus anasema jeshi la kulinda amani limweka mikakati ya kulinda raia.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa unasema kuwa kufikia sasa zaidi ya watu Elfu sitini wanapata hifadhi katika kambi za jeshi za kulinda amani na hali hii huenda ikasababisha hali ya Kibinadamu kuendela kuwa mbaya zaidi.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan Kusini na waasi wanaomuunga mkono aliekua makamo wa rais Salva Kiir, Riek Machar. 

Mapigano hayo yamesababisha mamia ya watu kupoteza maisha.