JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Kujiuzulu

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na waziri wake mkuu wajiuzulu

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia, anae tuhumia na Jumuiya ya Kimataifa kama chanzo cha machafuko ya kidini yaliyoibuka nchini humo, amejiuzulu, baada ya kushinikizwa na viongozi wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika ya kati katika mkutano aliyokua uliitishwa tangu jana hadi leo ijumaa, mjini N'Damena, nchini Chad.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu, Nicolas Tiangaye pia amejiuzulu. Nicolas Tiangaye , ambae alikua haafikiani na rais Michel Djotodia, na kusababisha mgawanyika katika taasisi za nchi wanatuhumiwa kua chanzo cha machafuko, ambayo yamesababisha mamia ya wtu wanapoteza maisha.

Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika ya Kati, ambao wamekua wakishirik mkutano huo, wamesema kuridhishwa na hatua ya kujiuzulu iliyochukuliwa na viongozi hao wawili.

Katika waraka uliyosainiwa na viongozi wa mataifa kutoka Afrika ya Kati, unampongeza Michel Djotodia na waziri wake mkuu, Nicolas Tiandaye, kwa kuikoa katika matatizo.

Malfu wa raia wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati wameadamana leo ijumaa asubuhi wakipinga kurejea kwa rais Michel Djotodia, ambae sasa anashiriki mkutano mjini N'Djamena, ambako kutachukuliwa uamzi kuhusu hatma yake.

Raia hao wamekua wamekusanyika pembezuni mwa tarafa ya Boy-Rabe, mbali kidogo na uwanja wa ndege, chini ya ulinzi wa wanajeshi wa Ufaransa na wanajeshi wa Kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca).

Waandamanaji hao wamekua wakisema “Djotodia ajiuzulu”.

“Tunataka Djotodia ajiuzulu. Inatakiwa mtu mwengine kuliongoza taifa hili”, amesema m'moja kati ya waandamanaji.

Tangu kupinduliwa kwa rais François Bozizé, mwezi wa machi mwa 2013, na kundi la waasi la Séléka , ambao wengi wao ni waislamu, wakiongozwa na Michel Djotodia, Jamuhuri ya Afrika ya Kati imejikuta imeingia katika machafuko ya kijamii na kidini.

Awali viongozi kutoka mataifa ya Afrika ya kati waliwapendekeza wabunge wa nchi hio kuandaa mkataba unaomuweka kando Michel Djotodia, na waziri mkuu, Nicolas Tiengaye, ili kukomesha machafuko yanayoendelea, jambo ambalo lilikua lilitupiliwa mbali na wabunge.

Katika ufunguzi wa mkutano wa kutathmini hatma ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Rais wa Chad Idriss Deby Itno, akiwa pia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati, alisema matumizi ya nguvu hayawezi kamwe kupewa kipau mbele dhidi ya utawala wa haki na kidemokrasia.

Ameendelea kuwa, unyanyasaji, mateso dhidi ya raia, mauaji ya wasio na hatia, na ubaguzi wa wageni lazima vikomeshwe.

Siku ya Alhamisi, rais Djotodia alionekana akishauriana na baadhi ya viongizi wa Seleka waliomsaidia kuipindua serikali ya aliyekua rais Francois Bozize.

Ikulu ya rais mjini Bangui inalindwa kwa sasa na wanajeshi wa Ufaransa.