JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Wabunge nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati hawakubaliani na madai ya kujiuzulu kwa rais Michel Djotodia

Wabunge wa nchini jamhuri ya Afrika ya kati
Wabunge wa nchini jamhuri ya Afrika ya kati assembleenationale

Wabunge 135 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wapo jijini Djamena nchini Chad wanakohudhuria mkutano maalum kuhusu hali ya usalama katika taifa lao. Mkutano huo unaongozwa na marais wa Jumuiya ya Afrika ya Kati, na wamekuwa wakimshinikiza rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia kujiuzulu kwa kile kinachoelezwa kuendelea kwake kuwa madarakani kunachangia kudorora kwa usalama nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanatarajiwa kupinga kura ya mabadiliko ya taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo hatima ya rais Djotodia.

Rais wa Chad Idriss Deby Itno, akiwa pia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati, amesema matumizi ya nguvu hayawezi kamwe kupewa kipau mbele dhidi ya utawala wa haki na kidemokrasia.

Ameendelea kuwa, unyanyasaji, mateso dhidi ya raia, mauaji ya wasio na hatia, na ubaguzi wa wageni lazima vikomeshwe.

Kwa upande wake Francois Bozize aliye kuwa rais kabla ya kufurushwa madarakani na waasi wa Seleka, amesema muda unawadia viongozi hao kurejesha utawala wa kidemokrasia na wa kikatiba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Rais Bozize amesema Djotodia na washirika wake lazima wawe na ujasiri wa kujiuzulu ili maamuzi yatakayotolewa yawe msingi mzuri kwa ajili ya viongo wapya watakaowekwa madarakani kwa njia ya kidemokrasia.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaomba viongozi hao kuweka mbele maslahi ya umma kuliko kupigania madaraka.

Siku ya Alhamisi, rais Djotodia alionekana akishauriana na baadhi ya viongizi wa Seleka waliomsaidia kuipindua serikali ya aliyekua rais Francois Bozize.