ISRAEL

Wa Israel wajiandaa kutoa heshima za mwisho kwa waziri mkuu wa zamani Ariel Sharon

Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon,enzi za uhai wake
Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon,enzi za uhai wake REUTERS/Gil Cohen Magen/Files

Wananchi nchini Israel leo Jumapili wanajiandaa kutoa heshima zao za mwisho kwa waziri mkuu wa zamani wa taifa hilo Ariel Sharon , ambaye amefariki dunia jana Jumamosi baada ya kupoteza fahamu kwa miaka minane.

Matangazo ya kibiashara

Sharon ambaye anasherehekewa na baadhi kama shujaa wa kijeshi,na wengine wakimtambua kama mwanasiasa aliyeendesha siasa za vitendo,huku maadui zake wakimwona kama mhalifu wa makosa ya jinai, Sharon alikuwa mtu wa mgawanyiko nyumbani na nje ya nchi yake.

Mwili wa Sharon huenda ukalazwa ikulu ya Israel ama kwenye ukumbi wa bunge kwa ajili ya zoezi la kutoa heshima za mwisho.
Mwili huo utazikwa kwa heshima za kijeshi Jumatatu mchana huko jangwa la Nagev Kusini mwa Israel

Viongozi mbalimbali duniani wametuma salamu za rambi rambi kwa taifa la Israel akiwemo rais wa Marekani Barack Obama ambaye amemwelezea Sharon kama kiongozi aliyeyatoa maisha yake kwa ajili ya taifa la Israel.