JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

Mchakato wa kumtafuta rais mpya wa mpito nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati waanza

RFI

Mamia ya wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliyo kua walitoroka jeshi hivi karibuni, wamerejea leo jumatatu katika makambi yao, ikiwa ni ishara ya kuanza kurejea kwa kwa hali ya utulivu, ambapo wanajeshi wa Ufaransa na wale wa kikosi cha Umoja wa Afrika wamezidisha ulinzi ili kukabiliana na waporaji.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la kiataifa la Mpito, ikiwa nibunge la mpito linakutana kesho katika kikao maalumu ili kumteua rais mpya wa mpito, atakae mrudilia mtangulizi wake Michel Djotodia, ambae Jumuiya ya kimataifa inamlaumu na waziri wake mkuu Nicolas Tiangaye kutowajibika vilivyo kwa kukomesha mauwaji ya kidini yaliyosababisha mamia ya watu kupoteza maisha.

Mabarabara ya mji mkuu Bangui yalifurika watu, ikilinganishwa na siku zingine. Usiku wa jana kuamkia leo ulikua tulivu, hapakuepo na wizi au uporaji, wamwthibitisha baadhi ya raia waliyokua wakihojiwa na AFP.

Raia hao wamebaini kwamba wanajeshi wa Ufaransa na wale wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca) walizidisha doria ili kutikomeza makundi ya waporaji ambao wanatumia mapanga na marungu.

Rais wa Baraza la Kitaifa la Mpito, akiwa pia rais wa mpito wa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Alexandre-Ferdinand Nguendet, amewatahadhari wapiganaji wa zamani wa Séléka na wanamgambo wa kikristo wa anti-balaka kua muda wa mapumziko umekwisha, atakae kutikana na hatia atahukumiwa kwa mujibu wa sheria.

Rais Nguendet ataongoza kesho kikao maalumu cha Baraza la Kitaifa la Mpito, ambacho kinao muda wa siku 15 ya kumteuwa rais mpya wa pito, ambae atakua mgombea kwenye uchaguzi wa urais baada ya kipindi cha miezi sita katika mwaka 2015.

Duru kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, zinafahamisha kwamba ,kunahitajika wagombea zaidi ya kumi, na bwana Nguendet atakua miongoni. Nguendet anapewa kipao mbele kuchukua wadhifa huo, kulingana na idadi kubwa ya wabunge(135) wanaomuunga mkono.