Kila upande nchini Sudan Kusini watoa masharti ili ushiriki moja kwa moja kwenye mazungumzo ya Addis-Ababa
Jeshi la Sudan Kusini limekua likiendesha kwa siku ya leo jumatatu mapigano dhidi ya waasi wanomuunga mkono aliekua makamu wa rais, Rieka Machar, ili kueweka katika himaya yake mji wa Bor, ambao unashikiliwa kwa muda wa wiki kadhaa na waasi. Hayo yanajiri wakati katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis-Ababa, mazungumzo ya kusaka amani kati ya pande mbili bado yanasuasua kuhusu swala la kuwaachia huru wahungwa waliyokaribu na upinzani.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mji wa Bor, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Jonglei (mashariki), bado uko mikononi mwa waasi, lakini jeshi letu linaendelea na juhudi za kuukomboa” Philip Aguer ameelezea AFP.
Tangu mapambano yaanze nchini Sudan kusini, mji wa mji mkuu wa jimbo la Jonglei, umeshashikiliwa mara tatu na pande mbili tofauti (jeshi na waasi), na kusababisha maelfu ya raia kuyahama makaazi yao.
Philip Aguer, hata waasi, wanathibitisha kwamba mapigano yaliripotiwa kati ya pande mbili jana jumapili alaasiri katika eneo linalopatikana kwenye umbali wa kilomita ishirini na mji wa Juba.
“Mapigano yalianza saa kumi (...) wakati (rais wa Sudan Kusini) Salva Kiir alituma idadi kubwa ya wanajeshi kwa kushambulia ngome zetu”, wamefahamisha waasi katika tangazo ambalo wametoa mjni Addis-Ababa, ambako kunafanyika mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya Sudan Kusini na waasi wanaomuunga mkono Riek Machar.
“ Gari liliokua linasafirisha wanajeshi lilichomwa moto, wakati ambapo mapigano hayo yalidumu saa mbili”, limeongeza tangazo hilo.
Philip Aguer, kwa upande wake, amefahamisha kwamba ni shambulio lililoendeshwa na wanajeshi wasiounga mkono serikali.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mapigano hayo yanaendelea kuathiri taifa hilo changa, tangu desemba 15 kutokana na kutoelewana kati ya rais Salva Kiir na makamu wa wake, Riek Machar, ambae aliamuachisha kazi katika mwezi wa julai mwaka jana. Mapigano hayo yamesababisha watu zaidi ya 1,000 kupoteza maisha na takribani 400,000 kuyahama makaazi yao.
Katika kitongoji cha Minkamman, kinachopatikana karibu kilomita 25 kusini magharibi mwa mji wa Bor, kuna wakimbizi wengi wa ndani, ambako zaidi ya watu 80,000 wanapewa hifadhi, huku watu 50,000 wakiwa wamekimbilia nchi jirani.
Salva Kiir aliwatuhumu wapinzani wake jaribio la mapinduzi, huku Riek Machar akikanusha madai hayo.
Hata hivo, mazungumzo yanaendelea, licha yakua bado yanasuasua kutokana na kwamba yanakabiliwa na pingamizi ya kusitisha mapigano kabla ya kuachiwa huru kwa wanasiasa waliyo karibu na Riek Machar, ambao wanaziwiliwa jela.
Waasi wanaomba kuachiwa huru kwa wanasiasa hao ili washiriki moja kwa moja katika mazungumzo, lakini serikali ya Juba inakataa, ikibaini kwamba lazima wahukumiwe.
Pande hizo mbili husika katika mgogoro wa Sudan Kusini wamekutana leo jumatatu kwa mazungumzo.
“Mazungumzo haya tunataraji kua yatazaa matunda na kusitisha mapigano, iwapo hakutatokea mambo mengine”, ameelezea AFP, kiongozi wa ujumbe wa serikali, Michael Makuei.
Ujumbe wa waasi haukutoa tangazo lolote.
Mwishoni mwa juma, wasuluhishi kutoka Afrika mashariki wakishirikiana na mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa kwa ajili ya Sudan Kusini, Donald Booth, walikutana kwa mazungumzo na Riek Machar katika sehemu ilosiri nchini Sudan Kusini.