SUDANI KUSINI-Mazungumzo

Wajumbe kutoka pande mbili hasimu nchini Sudan Kusini wakutana kwa mara nyingine mjini Addis-Ababa

RFI

Mazungumzo ya amani kati ya waasi na serikali ya Sudan Kusini yanarejelewa leo jijini Addis Ababa baada ya kuonekana kukwama jana kutoka na wajumbe kutofauatiana eneo la mazungumzo hayo. Mazungumzo hayo yalifanyika jana katika ukumbi wa Baa katika Hoteli ya Sheraton kutokana na kile kinachioelezwa kuwa wajumbe hao waliondolewa katika vyumba vya hoteli ya Sherathon vilivyochukuliwa na wageni kutoka Japan kutokana na ziara ya waziri mkuu wa Japan nchini humo Shinzo Abe.

Matangazo ya kibiashara

Kwa wiki kadhaa sasa mazungumzo hayo yamekuwa yakiendelea kwa mwendo wa kinyonga kutokana na kila upande kushiklia msimamo wake, upande wa waasi wanataka kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa kumi na mmoja wanaoshikiliwa na serikali ya Juba, shinikizo ambalo serikali imekataa.

Nchini Kenya raia wa Sudan Kusini wanaoishi katika taifa hilo hasa wale kutoka katika makabila ya Dinka na Nuer wameanza kutofatiana kuhusu machafuko yanayoendelea katika nchi yao.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mapigano nchini Sudan Kusini yanaendelea kuathiri taifa hilo changa, tangu desemba 15 kutokana na kutoelewana kati ya rais Salva Kiir na makamu wa wake, Riek Machar, ambae aliamuachisha kazi katika mwezi wa julai mwaka jana.

Mapigano hayo yamesababisha watu zaidi ya 1,000 kupoteza maisha na takribani 400,000 kuyahama makaazi yao.

Katika kitongoji cha Minkamman, kinachopatikana karibu kilomita 25 kusini magharibi mwa mji wa Bor, kuna wakimbizi wengi wa ndani, ambako zaidi ya watu 80,000 wanapewa hifadhi, huku watu 50,000 wakiwa wamekimbilia nchi jirani.

Salva Kiir aliwatuhumu wapinzani wake jaribio la mapinduzi, huku Riek Machar akikanusha madai hayo.

Mwishoni mwa juma, wasuluhishi kutoka Afrika mashariki wakishirikiana na mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa kwa ajili ya Sudan Kusini, Donald Booth, walikutana kwa mazungumzo na Riek Machar katika sehemu ilosiri nchini Sudan Kusini.