SUDANI KUSINI-Usalama

Zaidi ya watu 200 nchini Sudan Kusini wafa maji

RFI

Zaidi ya raia 200 wa Sudan Kusini waliyokua wakikimbia mapigano wamekufa maji , baada ya boti waliyokuwemo kuzama, msemaji wa jeshi Philip Aguer ameimbia AFP.“Tuna taarifa kwamba watu kati ya 200 na 300, wakiwemo wanawake na watoto wamekufa maji, baada ya boti waliyokuwemo kupinduka na kuzama majini”, amesema msemaji wa jeshi, akibaini kwamba watu hao walikuwa wanakimbia mapigano katika mji wa Malakalm mji mkuu wa jimbo muhimu la mafuta la Nil, kazkazini masharika.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, ajali hio imetokea leo asubuhi. Lakini vyombo vy habari vya Sudan kusini vimearifu kua ajali hio ilitokea usiku wa juzi jumapili kuamkia jana.

Mapigano yameshuhudiwa leo katika baadhi ya maeneo ya nchi. Waasi wameendesha mashambulizi mapya kwa kujaribu kuhibiti mji wa Malakal.

“Kuna mapigano ndani na pembezuni mwa mji wa Malakal”, amesema Toby Lanzer, mkuu wa shughuli za misaada kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa. Amebaini kwamba idadi ya wakimbizi wa ndani wanaopewa hifadhi katika ofisi ya Umoja wa Mataifa imeongezeka, ikitoka kwaq watu 10,000 hadi 19,000.

Jeshi kwa upande wake limefahamisha kwamba mapigano makali yanaripotiwa katika mji wa Bor, mji mkuu wa jimbo la Jonglei (mashariki). Mapigano hayo yalianza disemba 15, jeshi likijaribu kuurejesha kwenye himaya ya serikali, baada ya kushikiliwa na waasi.

“Tunaenda hadi Bor, kuna mapigano makali yaliyoanza tandu jana”, amesema Aguer.

Msemaji wa jeshi amekanusha habari kwamba waasi wameteka bandari ya Mongalla, inayopatikana karibu kilomita hamsini na mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kwenye barabara inayoelekea katika mji wa Bor.

“ Kwa sasa tuko kaskazini mwa Mongalla, tunadhibiti eneo lote”, amesema Aguer, akibaini kwamba mapigano makali yanaripotiwa kwenye umbali wa kilomita ishirini.

Tangu desemba 15, taifa changa la Sudan Kusini linakabiliwa na mapigano yaliyojitokeza baada ya kutoelewana kati ya rais Salva Kiir na alie kua makamu wake Riek Machar.

Mapigano hayo yamesababisha watu zaidi ya 1,000 kupoteza maisha na wengine 400,000 kuyahama makaazi yao.

Salva Kiir anawatuhumu wapinzani wake kwamba alikua wamepanga njama za kuipindua serikali yake, lakini Riek Machar anakanusha madai hayo, akibaini kwamba Salva Kiir ana lengo la kuwaangamiza wapinzani wake.