SYRIA-Wafadhili

Umoja wa Mataifa wasema, nchi ya Syria inahitaji msaada wa dharura kuwahudumia waathirika wa vita

RFI

Nchi wafadhili zinakutana leo jijini Coweit ili kukusanya takriban Dola za Marekani bilioni 6.5 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa vita vya Syria, kiwango ambacho Umoja wa Mataifa unasema ni muhimu kwa waathirika hao. Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamesababisha maalfu ya watu kupoteza maisha na wengine wengi kulazimika kuyahama makaazi yao,

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa na mashirika ya wahisani yamekuwa yakipiga kelele juu ya kupatikana kwa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kuwatolea msaada wa kibinadamu waathirika wa vita hivyo vilivyo gharimu hadi sasa maisha ya watu laki moja na elfu thelathini na wengine milioni 2.4 wakikimbia makwao.

Takriban nchi 24 zinakutana pamoja na masharika ya kimataifa chini ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon. Umoja wa Mataifa umesema, unahitaji dola za marekani bilionni 2.3 ili kuwasaidia watu milioni 9.3 raia wa Syria na dola za Marekani bilioni 4.2 kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi ambao wanakadiriwa kufikia milioni 4.1 katika mwaka huu wa 2014.

Kamishana wa Umoja wa Ulaya anaye husika na misaada ya kibinadamu Kristalina Georgieva amesema Umoja wa Ulaya utaongeza idadi yake ya msaada wa Euro milioni 165 kwa waathirika wa machafuko.

Amewatolea wito Jumuiya ya Kimataifa kufuata mfano wa Umoja wa Ulaya ambayo yao pekee imeitolea msaada nchi ya syria wa Euro bilioni 2 tangu mwanzoni mwa machafuko.