JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI-Diplomasia

Rais wa mpito nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Alexandre-Ferdinand Nguendet, hatogombea kwenye uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi

Laurent Correau / RFI

Wafadhili wa kimataifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamelitaka Baraza la Kitaifa la Mpito la nchi hio (CNT), ambalo ni bunge la mpito, kutoidhinisha majina ya watu kutoka upande wao watakaogombea kwenye uchaguzi ujao wa rais wa muda unotazamiwa kufanyika jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

“Jumuiya ya Kimataifa imelitaka Baraza la Kitaifa la Mpito kutochukua uamzi wowote unaohusiana na mchakato wa kumchaguwa rais mpya wa mpito”, amesema jenerali Noël Essongo, muakilishi wa msuluhishi katika mzozo wa Jamuhuri ya afrika ya Kati, rais wa Congo Denis Sassou Nguesso, akiwa pia mwenyekiti wa kamati ya ufundi inayofuatilia mchakato wa wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kamati hiyo inaundwa na Jumuiya ya Kimataifa, ikimaanisha wafadhili wa Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mzozo unaoikumba nchi hio, ikiwemo Ufaransa, Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrtika ya Kati (CEEAC).

Jumuiya ya kimataifa imetolea wito Baraza la Kitaifa la Mpito ichangie kwa kutoa masharti yanayohitajika na kutoruhusu watu wake kugombea kwenye uchaguzi, ambao utakua huru na wa haki, amesema jenerali Essongo katika tangazo liliyotolewa na ofisi ya msuluhishi.

Tangazo hilo linabaini kwamba ofisi ya msuluhishi na Jumuiya ya Kimataifa vimepongeza juhudi za Baraza la Kitaifa la Mpito, ambalo limekua likiandaa uchaguzi ili kumpata haraka iwezekanavyo rais wa mpito.

Bunge linapashwa kuidhinisha leo jumatano rasimu itakayo kuwa imetolewa na Baraza la Kitaifa la Mpito, ambayo inapendekeza hadi kesho alhamisi majina ya wagombea yawe yamekwisha wasilishwa, na uchaguzi ufanyike jumamosi.

Rais wa mpito, Alexandre-Ferdinand Nguendet, aliechukuwa nafasi ya Michel Djotodia aliejiuzulu hivi karibuni, amebaini leo kwamba hatagombea kwenye uchaguzi ujao ili kuepusha hali ya wasiwasi ambayo inaweza kujitokeza kutokana na kugombea kwake, na ataendelea kushirikiana na wengine kwa ujenzi wa taifa.

Mikataba ya kimataifa inapendekeza kua rais wa mpito hapashwi kugombea kwenye chaguzi za mwaka 2015