NIGERIA-Usalama

Watu 17 wauawa nchini Nigeria katika shambulio la kujitowa muhanga linaloshukiwa kuendeshwa na kundi la Boko Haram

RFI

Takriban watu 17 wamepoteza maisha katika shambulio linalo shukuwa kuendeshwa na kundi la Boko Haram katika soko moja jijini Maiduguri kaskazini mwa Nigeria, kiongozi wa kituo cha polisi cha Jimbo la Borno Lawan Tanko akisema kua watu 17 wamepoteza maisha huku wengine watano wakijeruhiwa katika shambulio la kujitowa muhanga na kuongeza kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Matangazo ya kibiashara

Upande wake msemaji wa jeshi nchini humo Muhamed Dole amesema wafuasi wa Boko Haram ambao wamepoteza muelekeo ndio wanaoshukiwa kutekeleza shambulio hilo, na kuongeza kuwa kumetokea idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha na wengine wengi wamejeruhiwa.

Kundi la Boko Haram limekua ni tishio kwa usalama wa eneo la kaskazini mwa Nigeria, likiishinikiza serikali kukubali sheria za kiisilamu kutumika katika eneo hilo ambako wakazi wake wengi ni waumini wa kiisilamu.

Kundi hilo limekua likitekeleza mashambulizi mbalimbali, kwenye makanisa, vituo vya polisi na jeshi.

Watu wengi wamepoteza maisha kutokana na mashambulizi yanoyotekelezwa na Boko Haram.

Kundi la Boko Haramu, limekiri kufanya shambulizi hilo.