MISRI-Kura ya maoni

Katiba mpya nchini Misri huenda ikapigiwa kura ya “Ndio”kwa asilimia zaidi ya hamsini.

RFI

Kura ya ndio kuhusu katiba mpya katika uchaguzi wa kura ya maoni uliofanyika juzi na jana nchini Misri unaelekea kutoa ushindi wa zaidi ya asilimia hamsini ya kura na utampa nafasi kwa kiongozi wa kijeshi nchini humo kuwania urais. Kura hiyo ya maoni juu ya katiba iliochapishwa na tume ilioteuliwa na jenerali Abdel Fattah al Sissi itampa nafasi ya kujilimbikizia madaraka zaidi kiongozi huyo wa kijeshi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa Jenerali Sissi ambaye ni kamanda wa majeshi, naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi ambaye tayari ametangaza nia yake ya kuwania uchaguzi iwapo katiba hiyo itaidhinishwa na wananchi kwa kuipigia kura ya ndio.

Juma moja kabla ya uchaguzi huo vyombo vya habari vimekuwa vikwatolea wito wananchi kupiga kura ya ndio badala ya kuipinga na ambapo wanasema kuipinga ni kuunga mkono ugaidi.

Wakati wa kampeni, wanaharakati 7 walitiwa nguvuni kwa tuhuma za kupiga kampeni kwa wananchi kuipinga katiba hiyo.

Licha ya hayo yote, hayakuzuia wananchi kupiga kura ya hapana.

Katiba hio mpya iliandaliwa, baada ya aliekua rais wa nchi hio Mohamed Morsi kuwekwa jela kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu, na anakabiliwa kifungu cha maisha jela.

Jenerali Abdel Fattah al-Sissi anatuhumiwa na wafuasi wa aliekua rais wa nchi hio Morsi kuhusika na mapinduzi ya serikali yake.