SYRIA-Diplomasia

Wafadhili na marafiki wa Syria wameahidi kuitolea Syria dola za kimarekani milioni 2.4.

Wafadhili na marafafiki wa Syria waliokutana nchini Kuwait wameahidi kutoa ahadi ya dola bilioni 2 nukta 4 kusaidia hali ya Kibinadamu nchini humo kutokana na machafuko yanayoendelea. Wajumbe kutoka Mataifa Sabini duniani na Mashirika 24 ya Kimataufa walikuatana jana jumatano chini ya uongozi wa katibu mkuu Ban Ki Moon ambaye alisema ahadi iliyotolewa haikufikia nusu ya fedha zinazohitajika ambazo ni zaidi ya dola Bilioni 6 kuwasaidia raia wa syria wanaoishi katika mazingira magumu.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Keryy amesema kua wananchi wa Syria watakavyonuifaika na msaada huu.

Umoja wa Mataifa na mashirika ya wahisani yamekuwa yakipiga kelele juu ya kupatikana kwa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kuwatolea msaada wa kibinadamu waathirika wa vita hivyo vilivyo gharimu hadi sasa maisha ya watu laki moja na elfu thelathini na wengine milioni 2.4 wakikimbia makwao.

Takriban nchi 24 zilikutana pamoja na masharika ya kimataifa chini ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon. Umoja wa Mataifa umesema, unahitaji dola za marekani bilionni 2.3 ili kuwasaidia watu milioni 9.3 raia wa Syria na dola za Marekani bilioni 4.2 kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi ambao wanakadiriwa kufikia milioni 4.1 katika mwaka huu wa 2014.

Awali, kamishana wa Umoja wa Ulaya anaye husika na misaada ya kibinadamu Kristalina Georgieva alisema Umoja wa Ulaya utaongeza idadi yake ya msaada wa Euro milioni 165 kwa waathirika wa machafuko, huku akitolea wito Jumuiya ya Kimataifa kufuata mfano wa Umoja wa Ulaya ambayo yao pekee imeitolea msaada nchi ya syria wa Euro bilioni 2 tangu mwanzoni mwa machafuko.