Uhalifu dhidi ya ubinadamu waripotiwa nchini Sudan Kusini
Mjumbe maalumu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa Ivan Simonovic amesema ameona miili iliyofungwa kwa pamoja na kupigwa risasi katika miji mbalimbali nchini Sudan Kusini, akibaini kwamba watalaamu 92 wa haki za Binadamu kutoka Umoja wa Mataifa wapo nchini humo kuendeleza uchunguzi wake na watatoa ripoti yao kwa kipindi cha wiki mbili zijazo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Umoja wa Mataifa unamtuhumu rais Salva Kirr na aliyekuwa Makamu wa rais Riek Machar kwa kutekeleza mauji makubwa na makosa mengine ya ukiukwaji wa haki za Binadamu kupitia vikosi vyao.
Jeshi la Uganda la UPDF limekiri kukabiliana na waasi wa Riek Machar wakati huu na hivi karibuni wanajeshi kadhaa wa uganda walipoteza maisha na waasi wengi wa Uganda waliuawa.
Uwepo wa majeshi ya Uganda upande wa serikali ya Juba, unapelekea hali ya mazungumzo huko Ethiopia kuendelea kupwaya. Kufuatia vile Uganda ni mwanachama wa Igad na sasa anaegemea upande mmoja.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa za kimataifa wanaona kuwa Igad imeshindwa, na sasa Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuingilia kati.