SYRIA-Mazungumzo

Hatimaye upinzani uliogawanyika nchini Syria wakubali kuhudhuria mazungumzo ya Geneva II

Wajumbe wa Muungano wa kitaifa wa upinzani nchini Syria
Wajumbe wa Muungano wa kitaifa wa upinzani nchini Syria news.yahoo.com

Upinzani uliogawanyika nchini Syria, hatimaye jana Jumamosi umefikia uamuzi wa kukubali kushiriki mazungumzo ya kimataifa kuhusu amani ya Syria,ukisema kwamba unataka kumwondoa rais Bashar Al Assad madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Muungano huo wa kitaifa ambao umegawanyika sana, umekuwa chini ya shinikizo kubwa la kimataifa kutaka wahudhurie mkutano huo, ambao una lengo la kutafuta njia ya kumaliza vita hiyo ya kikatili nchinihumo.

Serikali ya Damascus tayari imethibitisha kuhudhuria mazungumzo hayo,pamoja na kwamba waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani anaituhumu serikali kwa mbinu za kuhadaa ulimwengu akisema kuwa hakuna atakaye hadaika nazo.

Mazungumzo hayo ya kimataifa yanatarajia kuanza Januari 22 nchini Uswisi kwa lengo la kuanzisha serikali ya mpito ili kutafuta njia ya kumaliza vita vya kikatili ambayo imeua watu 130,000 na kuwafanya mamilioni kukimbia makazi yao tangu Machi mwaka 2011.