THAILAND-Maandamano

Marekani yatiwa hofu na hali ya usalama inayojiri nchini Thailand

Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa Marekani, Barack Obama RFI

Marekani imewaonya raia wake waishio Thailand kuwa makini na kinachoendelea nchini humo, huku kukiwa na ongezeko la machafuko ya kisiasa huko Thailand. Imearifiwa kuwa Kiasi ya watu 28 waliokuwa katika mkutano wa hadhara Jumamozi iliyopita wamejeruhiwa,7 miongoni mwao wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana kufuatia miripuko na kufyatuliwa kwa risasi katika ya jiji la Bangkok, nchini Thailand.

Matangazo ya kibiashara

Kitengo cha dharura kimesema mkasa huo umetokea katika sehemu ya maandamano yenye lengo la kushinikiza kuiondoka madarakani serikali ya taifa hilo.

Hili ni tukio la karibuni kutokea kufuatia mfululizo wa mashambulizi yanayofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya waandamanaji wanaoshinikiza kuondoka madarakani kwa Waziri Mkuu Yingluck Shinawatra.

Nchi ya Thailand imejikuta kwenye hali mbaya kisiasa toka kupinduliwa kwa waziri mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra miaka 7 iliyopita na sasa mdogo wake, Yingluck Shinawatra anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu akituhumiwa kuongoza nchi kwa kuzingatia matakwa ya ukoo wake.

Hofu imezidi kutanda nchini humo kufuatia shambulizi la hivi karibuni ambalo ni miongoni mwa matukio mabaya kushuhudiwa tangu kuanza kwa harakati za kuipinga serikali ya Yingluck.

Yingluck ameitisha uchaguzi mkuu mwezi ujao wa Februari, lakini wapinzani wanapinga upigaji kura wakihofia ushidni kushikiliwa tena na familia ya Shinawatra.