JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI-Dilpomasia

Umoja wa ulaya wakubali kutuma kikosi cha wanajeshi Jamhuri ya Afrika ya Kati

Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha wanajeshi kutoka mataifa ya Afrika Misca na Ufaransa, mjini Bangui
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha wanajeshi kutoka mataifa ya Afrika Misca na Ufaransa, mjini Bangui RFI

Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Ulaya wameidhinisha azimio la kuazisha operesheni ya kijeshi ya Umoja wa Ulaya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kuongeza nguvu kwa kikosi cha wanajeshi kutoka mataifa ya Kiafrika na wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini humo, vimefahamisha vyanzo vya kidiplomasia.

Matangazo ya kibiashara

“Kuna makubaliano kati ya mawazira kuhusu kuundwa kwa tume nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na makubaliano hayo yameafikiwa na mawaziri wote wa Ulaya”, kimefahamisha chanzo cha kidiplomasia.

Awaziri hao ambao wamekutana katika kikao leo mjini Brussels, wameafikiana nama watakabiliana na hali ya machafuko inayoendela. Baraza la majeshi ya Umoja wa Ulaya litapashwa kuandaa orodha ya mahitaji, na kutazama na mataifa wanachama uwezekanao wa kila m;moja kutoa mchango wake ili kikosi hicho kitumwe haraka iwezekanavyo.

Une source européenne a évoqué l'arrivée des premiers éléments sur le terrain fin février.

Duru kutoka katika kikao hicho zimefahamisha kwamba kundi la wanajeshi wa kwanza watawasili nchini Jamhuri ya afrika ya Kati mwishoni mwa mwezi wa februari.

Idadi ya wanajeshi kutoka mataifa ya Ulaya inaweza kufikia 500, ili kushirikiana na kikosi cha wanajeshi kutoka mataifa ya Afrika na wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini humo, kwa ulinzi wa mji wa Bangui, ukiwemo uwanja wa ndege.

Hadi sasa hakuna nchi ambayo imekwisha jitolea kuwatuma wanajeshi wake, kinyume na Astonia, ambayo itatuma wanajeshi 55.

Ufaransa ambayo ina wanajeshi 1,600, ilmependekeza iwe mwenyekiti wa “muungano wa mataifa” hayo ya Ulaya katika operesheni hio.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ubeljiji, Didier Reynders amesema katika kikao hicho kwamba, nchi yake tayari imetoa msaada wa vifa na mahitaji mengine kama vile chakula na maji katika operesheni ya kikosi cha wanajeshi hao kutoka Umoja wa Ulaya.

Ujeremani bado unatafakari uwezekano wa kutoa msaada wa kutosha, lakini uwezekano wa kutuma wanafeshi wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ulikua bado haujatiliwa maanani mapema leo jumatatu na viongozi wa Ujeremani.

Wakati huohuo, wabunge wanakutana kwa lengo la kumchagua rais wa mpito, huku ghasia zikiendelea kati ya waisilamu na wakristo.

Wagombea wanane wakiwemo meya wa mji mkuu Bangui pamoja na wana wawili wa marais wa zamani, ni miongoni mwa watu wanaowania wadhifa huo, kutaka kuchukua nafasi ya Michael Djotodia, alietakiwa na Jumuiya ya Kimataifa kuachia ngazi.

Duru ambazo zimetufikia punde , ni kwamba meya wa mji wa Bangui amechaguliwa kua rais wa mpito, akiwa na majukumu ya kwanza ya kurejesha hali ya utulivu na amani katika taifa hilo ambalo linakabiliwa na machafuko ya kidini.

Samba-Panza amechaguliwa katika kikao cha bunge, kwa kura 75 dhidi ya mpinzani wake ambae ni mwana wa rais wa zamani, Désiré Kolingba, aliepata kura 53.