Ukraine

Waandamanaji wajeruhiwa nchini Ukraine katika makabiliano na polisi

Wandamanaji wakikabiliana na polisi mjini Kiev, januari 19
Wandamanaji wakikabiliana na polisi mjini Kiev, januari 19 RFI

Maelfu ya waandamanaji nchini Ukaraine wamejeruhiwa kufuatia makabiliano kati yao na polisi wakati serikali ya nchi hiyo ikianza kutekeleza sheria ya kupiga marufuku mikusanyiko kwenye sehemu za umma. Waandamanaji wametupilia mbali hatua hio ya serikali ya kapiga marufuku mikusanyiko,

Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya usiku wa kuamkia leo mjini Kiev yanatajwa kuwa makubwa zaidi kufanywa na waandamanaji wa upinzani nchini humo ambao wanaendelea kukaidi makataa ya Serikali kuwataka kutofanya maandamano mjini Kiev na maeneo mengine ya Umma.

Polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya maelfu ya waandamanaji waliofurika mjini Kiev kupinga sheria iliyopitishwa na bunge nchini humo kukataza maandamano.

Magari ya polisi yalichomwa huku askari kadhaa wakijeruhiwa jirani kabisa na ukumbi wa bunge la nchi hiyo ambapi waandamanaji hao wanashinikiza rais Viktor Yanukovich kujiuzulu.

Umoja wa Ulaya na Serikali ya Marekani umeeleza kuguswa na nguvu kubwa ambayo inatumiwa na polisi kuwatawanya waandamanaji huku pia ukiitaka serikali ya nchi hiyo kutotekeleza sheria ya kukataza maandamano kwakuwa inalenga kuminya demokrasia na kutengeneza machafuko zaidi nchini humo.