SYRIA-Mazungumzo

Serikali ya Iran yautuhumu Umoja wa Mataifa kwa kuiondowa kwenye orodha ya nchi zitazoshiriki mazungumzo ya amani ya mjini Geneva Uswisi.

Mohammad javaz Zarif, waziri wa mambo ya nje wa Iran
Mohammad javaz Zarif, waziri wa mambo ya nje wa Iran

Serikali ya Iran kupitia waziri wake wa mambo ya nje  Mohammad javaz Zarif, imesema, imesikitishwa na hatuwa ya Umoja wa Mataifa kuinyang'anya mualiko wa kuhudhuria kwenye mkutano wa awamu ya pili ya Geneva kuhusu Syria na kuongeza kuwa mkutano huo unabahati ndogo za kufikia ufanisi. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon alilazimika kurejesha mualiko wa Iran kwenye mkutano huo kufuatia shinikizo kutoka kwa nchi wafadhili wa Syria pamoja na waasi kutishia kutoshiriki katika mkutano huo iwapo Iran itaalikwa..

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umetetea hatuwa yake hiyo kuwa serikali ya Iran imekataa kuunga mkono uundwaji wa serikali ya mpito nchini Syria, ndio sababu ya kuindowa kwenye orodha ya nchi zitazoshiriki mkutano huo.

Katika kile kinachoonekana ni ushindi kwa muungano wa upinzani nchini Syria, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, saa chache baada ya kutangaza kutoa mualiko kwa nchi ya Iran kuhudhuria mazungumzo ya Geneva, kiongozi huyo sasa amebadili msimamo wake na kutangaza kuiondoa nchi ya Iran kwenye mazungumzo hayo.

Upinzani nchini Syria awali ulitishia kujiondoa kwenye mazungumzo hayo iwapo nchi ya Iran ingeshirikishwa kwenye mazungumzo ya Geneva II, hatua ambayo upinzani ilidai Iran imekuwa mshirika wa katibu wa utawala wa rais Asad ikiwemo kutuma wanajeshi wake nchini Syria.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa UN, Martin Nesirky ndiye aliyetangaza uamuzi wa katibu mkuu Ban Ki Moon kuamua kuiondoa nchi ya Iran kwenye mazungumzo hayo kwa kile alichoeleza kuwa ni kigeugeu cha nchi ya Iran kuhusu mazungumzo hayo.

Nesirky amesema kuwa katibu mkuu Ban amesikitishwa na tangazo la ikulu ya Tehran kusema kuwa msimamo wake kwenye mazungumzo hayo unaweza kubadilika kwa kuwa hata mazungumzo ya awali hawakuunga mkono.

Serikali ya Urusi imejaribu kutetea mualiko wa Iran katika mazungumzo ya awamu ya pili ya mjini Geneva Uswisi baina ya wasi na serikali ya Syria.

Utawala wa Moscow kupitia waziri wake wa mambo ya nje Serguei Lavrov amesema kwamba kutoialika Iran ambayo ni mshirika wa karibu wa Syria kwenye mkutano wa awamu ya pili wa mjini Geneva Uswisi baina ya serikali ya rais Bashar Al Assad na waasi, ni kosa kubwa lisilo samehewa.

Wachambuzi wa siasa wanaona kwamba hakuna muafaka wowote utaopatikana katika mazungumzo hayo baada ya kuitenga Iran ambayo ni mshirika wa karibu wa Syria