Ukraine-Maandamano

Serikali ya Urusi yautuhumu Umoja wa Ulaya kuchochea machafuko yanayoendelea nchini Ukraine

Waandamanaji wakiapa kutoondoka kwenye maeneo wanayoshikilia, mjini Kiev
Waandamanaji wakiapa kutoondoka kwenye maeneo wanayoshikilia, mjini Kiev REUTERS/Gleb Garanich

Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov amewashtumu baadhi ya wanasiasa barani Ulaya kuchochea machafuko nchini Ukraine. Lavrov amesema ikiwa uchochezi huo utaendelea hali itaendelea kuwa mbaya nchini humo kutokana na machafuko yanayoendelea kwa sasa.

Matangazo ya kibiashara

Hapo jana polisi wa kutuliza ghasia mjini Kiev wameendelea kukabiliana na maelfu ya waandamanaji wa upinzani wanaoshinikiza kujiuzulu kwa rais Yanukovich kwenye.

Waandamanaji nchini humo wamekasirishwa na hatu ya rais Viktor Yanukoych kwa kutoingia katika Mkataba wa kibiashara na Umoja wa Ulaya.
Rais Yanukovich ameahidi kuzungumza na upinzani na waandamanaji hao ii kufikia mwafaka.

Rais wa Ukraine, Viktor Yanukovich amewaonya waandamanaji mjini Kiev na kuwataka kuondoka kwenye maeneo wanayoyakalia wakati huu maelfu ya polisi wakipelekwa kudhibiti hali ya usalama.

Maandamano ambayo yanaelezwa kuwa mabaya zaidi toka yalipoanza mwishoni mwa mwaka jana.

Hofu ya polisi kutumia nguvu zaidi kukabiliana na maandamano hayo imeendelea kutanda kwenye miji mbalimbali nchini humo kufuatia sheria iliyopitishwa na bunge juma hili inayoruhusu polisi kutumia nguvu kukabiliana na waandamanaji watakaokaidi amri ya kutakiwa kuondoka kwenye maeneo ya Kiev.

Kwenye tangazo lake kwa waandamanaji, rais Yanukovich amewataka wananchi hao kuondoka mjini kiev na kurejea majumbani mwao huku akionya kuwa kuendelea kwa maandamano hayo kunahatarisha usalama wa taifa zima.

Maelfu ya raia wanaendelea kufurika mjini Kiev kutoka miji mbalimbali wakiwa na mawe na mabomu ya kutengenezwa kwa mkono tayari kukabiliana na polisi wa kutuliza ghasia huku wakiapa kutoondoka kwenye maeneo wanayoyashikilia.