MISRI-Usalama

Milipuko mikubwa yatikisa mji wa Kairo nchini Misri

Watu watano wameuawa leo ijumaa katika milipuko mitatu, moja ambalo ilikua ni shambulio la kujitoa muhanga ambalo lmelenga makao makuu ya polisi mjini kairo. Mashambulizi hayo yanatokea katika mkesha wa maadhimisho ya miaka mitatu ya maandamano yaliyomng'atua madarakani alie kua rais wa taifa hilo Hosni Moubarak, huku serikali ya Misri ikiwa imeanzisha hivi karibuni harakati za kukabiliana na makundi ya waislamu wenye itikadi kali.

Makao makuu ya polisi kulikotokea shambulizi la mtu aliejitoa muhanga, mjini Kairo
Makao makuu ya polisi kulikotokea shambulizi la mtu aliejitoa muhanga, mjini Kairo RFI
Matangazo ya kibiashara

Mtu aliejitolea muhanga, ambae amekua akiendesha gari liliyobeba vilipuzi, aliharakia kugonga geti la makao makuu ya polisi na kusababisha maafa makubwa.

Mashambulizi dhidi ya polisi na jeshi yameongezeka tangu alipoondolewa madarakani rais wa kwanza aliechaguliwa kidemokrasia, Mohamed Morsi julai 3.

Mapema leo alfajiri, mtu aliekua akiendesha gari liliyokua limebeba vilipuzi alisubiri kwa muda mrefu askari polisi waondowe viziwizi kwenye barabara anayoelekea kwenye makao makuu ya polisi, mjni kati Kairo, na kuharakia kugonga geti la makao makuu ya polisi.

Mlipuko huo umeharibu sehemu kubwa ya makao makuu ya polisi pamoja na kuta za makavazi ya sana za dini ya kislamu, ambayo iko karibu na makao hayo makuu hayo ya polisi.

Kulingana na taarifa ya wizara ya afya, watu wanne wameuawa na wengine zaidi ya 70 wamejeruhiwa vikali.

Kwa muda wa saa tatu baadae, bomu ambalo halikua na nguvu, limelipuka kwenye barabara ya magari madogo na kusababisha kifo cha askari polisi m'moja na wengine wanne kujeruhiwa. Saa moja baadae, bomu lingine limelipuka mbele ya kituo cha polisi mjini Kairo.

Serikali iliyoko madarakani, iliyowekwa na kiongozi wa kijeshi, jenerali Abdel Fattah al-Sissi, imepiga marufuku maandamano tangu miezi saba iliyopita. Zaidi ya waandamanaji elfu moja, ambao wengi wao ni kutoka kundi la udugu wa kislamu (Muslim Brotherhood) waliuawa na maelfu walikamatwa na kuewekwa jela. Kundi hilo bado linamuunga mkono aliekua rais wa Misri Mohamed Morsi alieshinda uchaguzi tangu rais Hosni Moubarak ang'atuliwe madarakani.

Wakati huohuo zaidi ya wanajeshi 10 na wanajeshi wameuawa katika mashambulizi, ambayo kundi la Ansar Bait al-Maqdess lenye mafungamano na kundi la Al-Qaida, limekiri kutekeleza katika ukanda wa Sinaï, likidai kwamba ni ulipizaji kisasi dhidi ya mauwaji ya wafuasi wa Mohamed Morsi.

Serikali imelihusisha kundi la Udugu wa Kislamu na mashambulizi hayo, ikidai kwamba kundi hilo ni la kigaidi.

“Tunalani mashambulizi yaliyoutikisa mji wa Kairo, na kubali kwa nia njema kupambana kwa amani dhidi ya mapinduzi, umefahamisha leo ijumaa kupitia mtandao wa kijamii muungano unaomuunga mkono Mohamed Morsi, ambao unaongozwa na Muslim Brotherhood.

Mashambulizi hayo yanatokea wakati taifa la Misri likijianda kusheherekea hapo kesho jumamosi miaka mitatu ya harakati zilizomng'atua madarakani rais Hosni Moubarak.

Harakati hizo zilianza januari 25 mwaka 2011 katika baadhi ya mataifa ya kiarabu. Wanjeshi na askari polisi wamewekwa kwa idadi kubwa katika eneo la Tahrir, amabalo linajulikana kama kitovu cha ukombozi.

Wafuasi wa Morsi wamesema wataandamana kwa muda wa siku 18, lakini wawiri wa mambo ya ndani amewaonya wale wote watakaofanya maadamano kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.