JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Makabiliano

Juba na waasi watuhumiana kukiuka makubaliano ya usitishwaji vita

Serikali ya Juba na waasi, kila upande umekua ukimtuhumu upande mwengine kukiuka makubaliano ya usitishwaji mapigano, ambao uliwekewa saini na pande mbili husika siku mbili zilizopoita, ambao ungipelekea kusitisha mapigano kwa muda wa mwezi umoja, mapigano ambayo yameathiri taifa hilo changa kutokana na hali ya kutoelewana kati ya rais Salva Kiir na aliekua makamu wake Riek Machar.

Kambi moja ya raia wa Afrika ya Kati waliolazimika waliyoyahama makaazi yao
Kambi moja ya raia wa Afrika ya Kati waliolazimika waliyoyahama makaazi yao RFI
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayajakoma kikamilifu siku mbili baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa kusitisha mapigano kati ya serikali na wapinzani jijini Addis Ababa nchini Ethiopia ijumaa iliyopita.

Waziri wa Mambo ya nje wa Norway Borge Brende amesema hali haijawa thabiti na kuna umuhimu wa pande zote mbili kuhakiklisha kuwa vita vinakomeshwa zaidi ili kuheshimu mkataba huo.

Kwa mujibu wa Mkabata huo, wajumbe wa serikali na upinzani wanatarajiwa kukutana tena mjni Addis mapema mwezi ujao kuendelea na mzungumzo ya kutafuta suluhu la kisiasa.

Hali ya mamia ya raia imekua ngumu, na shirika la kimataifa linalohusika na watoto Unicef limefahamisha kwamba watoto thelatnini wamefariki kutokana na ugonjwa wa shurua.

Msemaji wa waasi, Lul Ruai Koang, amelishutumu jeshi la serikali kukiuka makubaliano ya usitishwaji mapigano, akibaini kwamba jeshi la serikali limekua likishambulia ngome zao katika jimbo la mafuta la Unity (kaskazini mwa nchi), pamoja na katika jimbo la Jonglei (mashariki).

“Jeshi letu limejihami baada ya kushambuliwa na jeshi la serikali”, amesema Lul Ruai Koang, katika taarifa iliyotolewa na jeshi.

Kwa upande wake jeshi limekanusha madai hayo, na kubaini kwamba waasi ndio wamekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.

Akihojiwa na kituo cha habari cha AFP kuhusu mapigano ambayo yanaendelea, msemaji wa jeshi, Philip Aguer, ametaja kutokua na taarifa ya mapigano ambayo yametokea.

Pande hizo mbili zimekua pia zikishutumiana kila upande kwamba hauwachunguzi wapiganaji wake katika maeneo ambako wako.

Machafuko nchini Sudan Kusini yamesababisha maefu ya watu kupoteza maisha na kulingana na ripoti iliyotolewa na waangalizi watu yumkini 10,000 na waliyo karibu na 700,000 wameyahama makaazi yao.

Takribani watu 76,000 wamepewa hifadhi kwenye makao makuu ya Umoja wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini kutokana na mchafuko hayo.