UKRAINE-Maandamano

Maandamano nchini Ukraine yasambaa katika maeneo mengine ya nchi

Waandamanaji wakiapa kuendelea na maandamano, mjini Kiev
Waandamanaji wakiapa kuendelea na maandamano, mjini Kiev RFI

Maandamano nchini Ukraine yamesambaa na kutoka nje ya jiji la Kiev na sasa yameelekea Kaskazini, Kusini na Mashariki mwa nchi hiyo. Jijini Kiev waandamanaji wanaomtaka rais Viktor Yanukovich kujiuzulu wamezuia barabara kuu pamoja na barabara inayoelekea kwenye jango la wizara ya Haki. Kongozi wa upinzani Arse niy Yatse nyuk amekataa ombi la rais Yanukovych kumteua Kama Waziri Mkuu.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hao wanasema wataendelea na maandamano hayo hadi pale rais Yanukovich atakapojiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya.

Maadamano hayo yalianza mwaka uliopita baada ya rais Yanukoch kukataa kutia saini mkataba wa Kibiashara na Umoja wa Ulaya.

Wapinzani nchini Ukraine wameapa kuendelea na maandamano dhidi ya serikali ya Rais Viktor Yanukovych mpaka matakwa yao yatakapokamilika licha ya rais huyo kutoa nafasi za juu za uongozi kwa viongozi wa upinzani.

Juzi jumamosi, rais Yanukovich alitangaza kutoa nafasi ya waziri mkuu na naibu waziri mkuu viongozi wakuu wa upinzani Arseniy Yatsenyuk pamoja na Vitali Klitschko ili kujaribu kutafuta suluhu ya machafuko hayo yaliyodumu kwa takribani miezi miwili.

Wakizungumza na maelfu ya waandamanaji mjini Kiev, viongozi hao wa wapinzani walisema lengo lao sio tu nafasi za uongozi serikalini bali ni kutaka taifa hilo lijiunge na ushirikiano wa kiuchumi na Umoja wa Ulaya EU.

Bado haijafahamika kama viongozi hao watakubali kushika nyadhifa hizo ama watazikataa na kuendeleza harakati zao.

Umoja wa Ulaya umeomba zichukuliwe hatua madhubuti kusitisha ghasia hizo, ambazo kwa mujibu wa wanaharakati tayari zimesababisha vifo vya watu watano na huenda hali ikawa mbaya zaidi endapo Rais Viktor Yanukovich ataamua kutumia nguvu zaidi kukabiliana na makundi ya waandamanaji walioingia mitaani takribani miezi miwili sasa.

Polisi wameendelea kukabiliana na waandamanaji katika mji mkuu wa nchi hio Kiev wakitumia risasi za mipira na mabomu ya kutoa machozi, hatua ambayo haijaonekana kufua dafu katika kutuliza ghasia.