MAREKANI-SOMALIA-Mashambulizi

Marekani yaanzisha operesheni ya kumsaka m'moja kati viongozi wa nagazi ya juu wa al-Qaida nchini Somalia

Ndege ya jeshi la Marekani isiyotumia rubani, kusini mwa Somalia
Ndege ya jeshi la Marekani isiyotumia rubani, kusini mwa Somalia RFI

Jeshi la Marekani limeshambulia ngome ya wanamgambo wa Al Shabab nchini Somalia ili kuhakikisha kua limemuangamiza kiongozi wa ngazi ya juu wa kundi hilo anaeishi nchini Somalia, wamethibitisha maafisa wa ngazi ya juu kwenye wizara ya ulinzi ya Marekani. Wizara ya Ulinzi ya Marekani inasema jeshi lake limetumia ndege zisizotumia rubani kuwashambulia ngome ya wanagambo hao.

Matangazo ya kibiashara

“mashambulizi haya ambayo tumeanzisha yanamlenga kiongozi wa ngazi ya juu wa kundi la al-Shabab, amesema m'moja wa maafisa hao ambae hakutaka jina lake litajwe, wakati alipokua akihojiwa na kituo cha habari cha AFP kuhusu mashambulizi hayo yaliyotekelezwa na jeshi la Marekani katika bandari ya Barawe, kusini-mashariki mwa Somalia.

Afisa huyo amejizuia kuthibitisha jina la kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa al-Shabab ambae anasakwa, huku akibaini kwamba jeshi la Marekani limeanza uchunguzi li kujua iwapo limefikia malengo yake.

“Uchunguzi umeanzishwa ili kujua iwapo makombora tuliyovurumisha yameuangamiza muhusika”, amesema afisaa mwengine.

Hili ni shambulizi la pili linalofanywa na Marekani katika siku za hivi karibuni dhidi ya wanamgambo hao ambao wanaendelea kua hatari kwa usalama nchini Somalia na nchi za Arika Mashariki.

Operesheni ilianzishwa siku mbili baada ya al-Shabab kutolea wito makundi ya waislamu wenye itikali wenye mafungamano na kundi la al-Qaida, dhidi ya wanajeshi wa kigeni, baada ya Ethiopia kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (Amisom) ambacho kinakabiliana na makundi ya waislamu weye itikadi kali ya kidini.

Viongozi wa ngazi ya juu wa al-Shabab, akiwemo kiongozi mkuu wa kundi hilo, Ahmed Abdi Godane, walikutana kwa mazunguzo wiki jana kabla ya kutoa tangazo hilo linalohusiana na Ethiopia, msemaji wa al-Shabab, Ali Mohamud Rage, ameiambia AFP.

Marekani imewatuma hivi karibuni washauri wa kijeshi nchini Somalia ili kuzidisha usaidizi kwa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika kinachokabiliana na wanamgambo wa kundi la a-Shabab na makundi mengine yenye mafungamano na al-Qaida.

Kikosi hicho cha Marekani kiliyotumwa nchini Somalia ni cha kwanza, toka Marekani iwakose wanajeshi wake 18 waliyouawa katika ajali ya helikopta ya kijeshi aina ya Blackhawk iliyodunguliwa katika mwaka 1993 wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vipokua vikirindima.