UKRAINE-Bunge

Ukraine : waziri mkuu ajiuzulu, sheria inayopiga marufuku maandamano yafutwa

Kwenye jengo la Bunge nchini Ukraine, 28 januari 2014
Kwenye jengo la Bunge nchini Ukraine, 28 januari 2014 REUTERS/Gleb Garanich

Bunge la Ukraine limechukua uamzi wa kufuta sheria iliyokua inapiga marufuku maandamano yaliyopelekea raia wa Ukraine kuandamana wakiunga mkono nchi hio kujiunga na Umoja wa Ulaya. Wabunge 361 wameidhinisha uamzi wa kufuta sheria hio iliyokosolewa vikali na mataifa ya kimagharibi kama ukiukwaji wa wa uhuru wa mwananchi, lakini wabunge wawili pekee, wamepinga uamzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Kikao cha bunge kimeahirishwa saa chache baadae hadi saa nane saa za kimataifa, ambapo wabunge watajadili uwezekano wa kutoa msamaha kwa waandamanaji waliyokamatwa wakati wa makabiliano na polisi.

Sheria hiyo iliyokua inapiga marufuku maandamano ilikua imependekeza adhabu hadi kifungo cha miaka mitano jela kwa waliyoandamana na kuzorotesha shughuli za serikali, na kutozwa faini ao kifungo kulingana na sheria za uongozi kwa waandamanaji waliyoandamana wakivalia kofia ngumu, ambao ndio wengi wakiandamana mjini Kiev.

Sheria hio ilikua inapendekeza pia kazi zenye maslahi ya umma kwa wale ambao watakutikana wameandika kwenye tovuti habari zozote zinazohusiana na hali inayojiri nchini Ukraine.

Maadamano makubwa yalishuhudiwa wakati sheria hio ilipoidhinishwa na kusababisha vifo vya watu yumkini watatu katikati mwa mji wa Kiev.

Maandamano hayo yalisambaa katika maeneo mengine ya nchi, na shughuli zilizorota katika baadhi ya mikoa ya magharibi na kukwamisha kazi za wakuu wa mikoa waliyokua wameteuliwa na Viktor Ianoukovitch.

Uamzi huo wa kubadili sheria hio umechukuliwa katika kikao cha bunge kiliyoitshwa katika hali ya kutafutia suluhu mgogoro uliyoanza tangu zaidi ya miezi miwili iliyopita, baada ya rais wa Ukraine kukataa kusaini mkataba wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya, na badala yake akaamua kushirikiana na Urusi.

Waziri mkuu wa Ukraine Mykola Azarov amewasilisha mapema leo asubuhi barua ya kujiuzulu.