TANZANIA-UFARANSA-Mlima Kilimanjaro

Raia watano wenye ulemavu kutoka Ufaransa na Tanzania wakwea kwa mara ya kwanza mlima Kilimanjaro

Wafaransa wasioweza kuona wakikwea Mlima Kilimanjaro Tanzania
Wafaransa wasioweza kuona wakikwea Mlima Kilimanjaro Tanzania RFI

Deogratius Chami anaweka historia kwa kuwa mtanzania wa kwanza mwenye ulemavu kuukwea mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zadi barani Afrika. Chama mwenye umri wa miaka 29 mkaazi wa Moshi na mwenye ulemavu wa kupooza anaandamana na walemavu wengine wanne kutoka Ufarasna wasiokuwa na uwezo wa kuona wala kusikia, ambao ni Jean Christian, Joseph, Maria na Alain.

Matangazo ya kibiashara

Safari hii imefadhiliwa na chama cha walemavu kutoka Ufaransa cha Chemindessens chenye makao yake makuu mjini Grasse kikishirikiana na Chama cha Wasioona cha Ile de France (ARAM), na Chami anasaidiwa na wataalam kuukwekwea mlima huo kwa kutumia kiti maalum cha magurudumu.

Akizungumza na RFI Kiswahili, wakati akianza kuukwea mlima huo siku ya Jumamosi , Chami aliyepata ajali akiwa kijana mdogo na kuwa mlemavu alisema hatimaye ndoto yake ya kukwea mlima huo imetimia hasa kuwa mtanzania wa kwanza mwenye ulemavu kufanya hivyo.

Safari ya kufika kileleni mwa Mlima Kilimanjaro ni ya siku saba na lengo la safari hii ni kuihamasihsa jamii juu ya ulemavu , uwe ni wa kupooza au wa viungo vya mwili.

Watu hao wenye ulemavu kutoka Ufaransa na Tanzania wamebuni neno Kilihandy (Kili inamaanisha Kilimanjaro na Handy ikimaanisha Ulemavu), lengo likiwa ni kupanda mlima huu mrefu kuliko yote barani Afrika ili kuonesha kuwa pamoja na tofauti za Kijiografia na kitamaduni, watu wanaweza kushirikiana kuifanya dunia kuwa na mshikamano zaidi.

Kilihandy ni ndoto ya Deogratius, aliepooza na anaeshi katika mitelemko ya mlima Kilimanjaro ambae amekua na shauku ya kuiangalia dunia akiwa juu ya mlima huu....

Kilihandy ni ndoto ya Joseph aliyezaliwa akiwa kiziwi kisha kopofoka ukubwani. Alipokua mtoto, alipata kujifunza na kujenga mawazoni mwake taswiraya bara la Afrika, japo hawezi kuona mandhari, anatamani akanyage ardhi yake....

Kilihandy ni ndoto ya Alain na Jean-Christian, ambao kwa miaka kadhaa wamezunguka karibu dunia nzima, hata hivyo maisha yamewabadilikia baada ya kuwa vipovu. Huu ni mwanzo wa maisha yao katika hali waliyonayo....

Kilihandy ni ndoto ya Maria, ambae licha ya kutoona vizuri, hakuwahi kukata tamaa ya kuendelea kujifunza mengi yanayopatikana katika sayari hii.....

Kilihandy ni ndoto ya kila siku ya wote watakaowasaidia watu hao wenye ulemavu katika kutimiza ndoto zao kwa kuwafanya watambue kuwa hata kama ulimwengu unatazamwa kwa namna tofauti, ulemavu wa mtu haumfanyi awe tofauti na watu wengine.