JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Diplomasia

Kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Ulaya kinatazamiwa kutumwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa RFI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuruhusu Umoja wa Ulaya kutuma wanajeshi wake wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ufaransa kupitia kwa balozi wake katika Umoja huo Gerard Araud amesema wanajeshi elfu kumi wanahitajika kutumwa nchini humo ili kusaidiana na wale wa Afrika na Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Rais Catherine Samba Panza ameomba rasmi Umoja wa Mataifa kuwatuma wanajeshi zaidi nchini mwake kutokana na machafuko yanayoendelea.

Rais catherine Samba-Panza amemteua hivi karibuni waziri mkuu, ambae hakuchelewa kuunda serikali inayoundwa na mawaziri ishiri, wakiwemo wanawake saba. Waasi wa zamani wa Seleka na wanamgambo wa kundi la wakristo la Anti-balaka walishirikishwa katika serikali hio mpya, licha ya kundi hilo la Anti-balaka kubaini kwamba, hawakushirikishwa vilivyo katika serikali mpya.

Rais Samba -Panza alichukua na fasi ya mtangulizi wake, Michel Djotodia aliekua akiungwa mkono na waasi wa Seleka, baada ya Jumuiya ya Kimataifa kumtaka ajiuzulu yeye na waziri wake mkuu Nicolas Tiangaye aliekua anaungwa mkono na wanamgambo wa kundi la wakristo la Anti-balaka, ili kutazama jinsi ya kukomesha machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Waasi wa Seleka, ambao wengi wao ni waislamu walichukua madaraka, baada ya kuungsha utawala wa Francois Bozize, wakimtuhumu kwamba alikua hatendei haki raia wake.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine zaidi ya 400,000 kuyahama makaazi yao.