SYRIA-Mazungumzo

Syria : Mazungumzo ya amani kuhusu Syria yarejelewa baada ya kukwama

RFI

Mpatanishi wa Kimataifa wa mzozo huo Lakdhar Brahimi amesema kuwa hakuna chochote kilichopatikana katika siku ya nne ya mazungumzo yanayowashirikisha wajumbe wa serikali ya Syria na wale wa upinzani mjini Geneva, huku akiasema kwamba juhudi zinaendelea ili angalau kupata muafaka kuhusu uundwaji wa serikali ya mpito. Mazungumzo hayo ameonekana kukwama jana baada ya kujitokeza mvutano kuhusu serikali ya mpito.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa serikali ya Syria jana waliwasilisha azimio wakati wa mazungumzo hayo kuishtumu Marekani kuendelea kuingilia maswala ya syria huku, upinzani ukisema serikali haijaleta chochote katika meza ya mazungumzo na imekataa kutekeleza makubaliano ya wanawake na watoto kuondoka katika mji wa Homs.

Awali serikali ya Syria ilitoa tangazo liliyosomwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambamo iliruhusu raia waishio katika mji wa Homs kuondoka, baada ya miezi kadhaa kutoondoka katikaq mji huo.

Mazungumzo hayo kati ya wajumbe wa serikali ya Syria na wale wa upinzani yalianza rasmi ijumaa ya juma liliyopita mjini Geneva, huku kukishuhudiwa mvutano kati ya pande mbili.

Upinzani umekua ukipendekeza rais Bachar al-Assad ajiuzuli, huku serikali ikitupilia mbali pendekezo hilo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon aliikua alialika Iran katika mazungumzo hayo, lakini baadae alibadili msimamo wa kunyanganya aliko Iran, baada ya upizani kususia kushiriki kwenye mazungumzo. Urusi ililani uamzi huo wa katibu mkuu wa kuinyanganya aliko Iran, na kubaini kwamba Ban alionyesha udhaifu fulani katika juhudi zake za kutafutia ufumbuzi mgogoro wa Syria.