UKRAINE-Bunge

Ukraine : Bunge lajadili hatma ya waandamanaji wanaoziwiliwa

RFI

Wabunge nchini Ukraine wanatarajiwa kujadili na kupigia kura kusamehewa kwa mamia ya waandamanaji wa upinzani wanaozuiliwa. Rais Viktor Yanukovych anasema wafungwa hao wanaweza kusamehewa tu ikiwa waandamnaji wataacha maandamnao na kuondoka katika majengo ya serikali. 

Matangazo ya kibiashara

Upinzani ambao pia umepanga maaandamano makubwa hivi leo, umekataa ombi hili la rais Yanukovych na kuendelea na shinikizo zake za kumtaka ang'atuke madarakani na kuitisha uchaguzi wa haraka.

Jana Wazir Mkuu Mykola Azarov alijiuzulu kutokana na shinikizo za waandamanaji.

Bunge la Ukraine lilichukua hivi karibuni uamzi wa kufuta sheria iliyokua inapiga marufuku maandamano yaliyopelekea raia wa Ukraine kuandamana wakiunga mkono nchi hio kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Wabunge 361 walidhinisha uamzi wa kufuta sheria hio iliyokosolewa vikali na mataifa ya kimagharibi kama ukiukwaji wa wa uhuru wa wananchi, lakini wabunge wawili pekee, walipinga uamzi huo.

Sheria hiyo iliyokua inapiga marufuku maandamano ilikua imependekeza adhabu hadi kifungo cha miaka mitano jela kwa waliyoandamana na kuzorotesha shughuli za serikali, na kutozwa faini ao kifungo kulingana na sheria za uongozi kwa waandamanaji waliyoandamana wakivalia kofia ngumu, ambao ndio wengi wakiandamana mjini Kiev.

Sheria hio ilikua inapendekeza pia kazi zenye maslahi ya umma kwa wale ambao watakutikana wameandika kwenye tovuti habari zozote zinazohusiana na hali inayojiri nchini Ukraine.

Maadamano makubwa yalishuhudiwa wakati sheria hio ilipoidhinishwa na kusababisha vifo vya watu yumkini watatu katikati mwa mji wa Kiev.

Maandamano hayo yalisambaa katika maeneo mengine ya nchi, na shughuli zilizorota katika baadhi ya mikoa ya magharibi na kukwamisha kazi za wakuu wa mikoa waliyokua wameteuliwa na Viktor Ianoukovitch.

Uamzi huo wa kubadili sheria hio ulichukuliwa katika kikao cha bunge kiliyoitshwa katika hali ya kutafutia suluhu mgogoro uliyoanza tangu zaidi ya miezi miwili iliyopita, baada ya rais wa Ukraine kukataa kusaini mkataba wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya, na badala yake akaamua kushirikiana na Urusi.