JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Diplomasia

Amnsesty international inachunguza mauaji ya raia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Raia wakiwazika ndugu zao waliyouawa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Raia wakiwazika ndugu zao waliyouawa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati RFI

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linachunguza mauaji ya raia ya hivi karibuni katika mji wa Bour katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na makabiliano ya kidini. Mwakilishi wa shirika la Amnesty International nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, Donatella ROVERA, amesema kuna ulazima idadi ya vikosi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati iongezwe.

Matangazo ya kibiashara

“Kwanza lazima kuwepo na kuwasili kwa vikosi vyote vilivyoahidiwa, lakini pia lazima kuhakikisha kuwa askari waliopo hapa watoke kwenye makambi yao na kuwaomba askari hao wafanye kazi iliyowaleta hapa, hususan ulinzi wa raia”, amesema Donatella ROVERA.

Jijini Addis Ababa Ethiopia marais wa Umoja wa Afrika wanakuatana na miongoni mwa maswala nyeti yatakayojadiliwa ni pamoja na usalama nchini humo.

Mwenyekiti wa baraza la Usalama la Umoja wa Afrika, rais Alpha Conde, amesema mataifa ya Afrika yataendelea kuunga mkono mchakato wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

“Uko umuhimi wa kuunda mchakato wa kusindikiza taasisi za mpito kwa ajili ya kuelekea maandalizi ya Uchaguzi ndani ya muda unaokubalika. Hatuna budi kufanya hivyo ili kuokoa nchi hiyo na hatari ya machafuko yasiyo na kikomo na yanayoweza kusababisha mauwaji ya kimbari. Hatuna budi kufanya hivyo ili kuruhusu amani ya kudumu kwa nchi hiyo na kuwezesha wananchi wa jamhuri ya Afrika ya kati kupatanishwa kati yao na kujenga demokrasia kwa ajili ya ujenzi wa taifa iliyositawi” amesema rais Conde.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha maelfu ya raia kupoteza maisha na mamia kwa maelfu kuyahama makaazi yao.