THAILAND-Uchaguzi

Thailand : Thailand yajiandalia uchaguzi

Waziri mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra
Waziri mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra RFI

Serikali ya Thailand inasema itatuma maelfu ya maafisa wa usalama kote nchini kuhakikisha kuwa kuna usalama wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mkuu siku ya Jumapili. Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema uchaguzi huo wa jumapili huenda usimalize machafuko yanayoendelea hasa baada ya upinzani kusema watashirki.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji kwa miezi kadhaa sasa wamekuwa wakimshinikiza waziri mkuu Yingluck Shinawatra kujiuzulu kutokana na serikali yake kuendelea kupata ushauri kutoka kwa kaka yake Thaksin Shinawatara , shinikizo ambazo amekataa na badala yake kuitisha uchaguzi mkuu.

Nchi ya Thailand imejikuta kwenye hali mbaya kisiasa toka kupinduliwa kwa waziri mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra miaka 7 iliyopita na sasa mdogo wake, Yingluck Shinawatra anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu akituhumiwa kuongoza nchi kwa kuzingatia matakwa ya ukoo wake.

Hofu imezidi kutanda nchini humo kufuatia shambulizi la hivi karibuni ambalo ni miongoni mwa matukio mabaya kushuhudiwa tangu kuanza kwa harakati za kuipinga serikali ya Yingluck.

Awali upinzani ulipinga kushiriki kwenye uchaguzi ukihofia ushindi kushikiliwa tena na familia ya Shinawatra.