UKRAINE-Maandamano

Bunge laidhinisha mswada wa kutoa msamaha kwa waandamanaji wanaoshikiliwa nchini Ukraine

Kikao cha bunge nchini Ukraine, januari 29
Kikao cha bunge nchini Ukraine, januari 29 RFI

Wabunge nchini Ukraine wamepitisha mswada wa kutoa msamaha kwa mamia ya waandamanaji wanaoshikiliwa naserikali. Hata hivyo upinzani ulisusia upigaji kura kutoka kwa mswada huo kueleza kuwa wafungwa hao wataachiliwa tu baada ya wapinzani kuacha kuandamana na kuondoka katika majengo ya serikali.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji katika jiiji la kiev pia wamekataa mswada huo na kusema wataendelea kuandamna na kupiga kambi katika majengo ya serikali na kuendela kushinikiza kujiuzuliu kwa rais Viktoir Yanukovych wakisema amekataa kutia saini mkataba wa biashara na Umoja wa Ulaya.

Awali rais Viktor Yanukovych alisema wafungwa hao wanaweza kusamehewa tu ikiwa waandamnaji wataacha maandamnao na kuondoka katika majengo ya serikali,
ombi ambalo lilipingwa na upinzani ukimtaka la rais Yanukovych ang'atuke madarakani na kuitisha uchaguzi wa haraka.

Juzi Wazir Mkuu Mykola Azarov alijiuzulu kutokana na shinikizo za waandamanaji.
Bunge la Ukraine lilichukua hivi karibuni uamzi wa kufuta sheria iliyokua inapiga marufuku maandamano yaliyopelekea raia wa Ukraine kuandamana wakiunga mkono nchi hio kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Wabunge 361 walidhinisha uamzi wa kufuta sheria hio iliyokosolewa vikali na mataifa ya kimagharibi kama ukiukwaji wa wa uhuru wa wananchi, lakini wabunge wawili pekee, walipinga uamzi huo.

Sheria hiyo iliyokua inapiga marufuku maandamano ilikua imependekeza adhabu hadi kifungo cha miaka mitano jela kwa waliyoandamana na kuzorotesha shughuli za serikali, na kutozwa faini ao kifungo kulingana na sheria za uongozi kwa waandamanaji waliyoandamana wakivalia kofia ngumu, ambao ndio wengi wakiandamana mjini Kiev.

Sheria hio ilikua inapendekeza pia kazi zenye maslahi ya umma kwa wale ambao watakutikana wameandika kwenye tovuti habari zozote zinazohusiana na hali inayojiri nchini Ukraine.

Maadamano makubwa yalishuhudiwa wakati sheria hio ilipoidhinishwa na kusababisha vifo vya watu yumkini watatu katikati mwa mji wa Kiev.

Maandamano hayo yalisambaa katika maeneo mengine ya nchi, na shughuli zilizorota katika baadhi ya mikoa ya magharibi na kukwamisha kazi za wakuu wa mikoa waliyokua wameteuliwa na Viktor Ianoukovitch.

Uamzi huo wa kubadili sheria hio ulichukuliwa katika kikao cha bunge kiliyoitshwa katika hali ya kutafutia suluhu mgogoro uliyoanza tangu zaidi ya miezi miwili iliyopita, baada ya rais wa Ukraine kukataa kusaini mkataba wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya, na badala yake akaamua kushirikiana na Urusi.